Back

ⓘ Tala (goddess)
Tala (goddess)
                                     

ⓘ Tala (goddess)

Tala, kutokana na mungu wa Kihindu Tara, ni jina la mungu wa kike ambaye ni nyota ya asubuhi na jioni katika hadithi za Kitagalogi. Asili yake inategemea kulingana na mkoa. ambapo kuna Golden Tara, sanamu ya dhahabu ya Majapahit.Mnamo mwaka 1918 eneo la Agusan rasmi iligunduliwa Tala. Shujaa wa Tala ana uwiano karibu sana na hadithi kati ya tamaduni zisizo za kiFilipino kama vile kwa India makabila kama ya Bihar, Savara na Bhuiya, pamoja na Indianized Semang.

Hadithi nyingi zinaelezea zaidi kuwa Tala ni mmoja wa binti watatu wa Bathala kwa mwanamke anayekufa. Dada wa Tala ni pamoja na Mayariambaye ni mungu wa mwezi na Hanan hujulikana kama mungu wa asubuhi. zaidi anajulikana kuwa aliunga mkono kuundwa kwa kikundi cha jadi cha Tagalog. Tala alitumia kifaa mithili ya duara nyepesi kusafirisha wanaume kwenda usiku. Tafsiri za Asili ya hizi vifaa vilivyotumika kusafirisha ilibadilishwa kugunduliwa kama viumbe hatari ambavyo vinaua wanaume au kufanya wanaume kusahau njia zao, kwa ushawishi wa kitamaduni na kimila iliyochochewa na Uhispania.

Katika hadithi nyingine ambazo ni za kisasa zaidi, mungu wa jua Arao Apolaki na mungu wa mwezi Buan Mayari hawa wote walikuwa pamoja na familia kubwa za nyota, ingawa Buan aliamini nyota zake haziwezi kuishi katika joto la Arao. Baadae wote wawili walikubaliana kuharibu nyota zao, wakati huo Arao aliamua kula yake, huku Buan aliificha Nyota yake katika mawingu, tegemeo ambapo mara kwa mara wangeibuka.Hatma yake Arao alijawa na ghadhabu huku akiendelea kumtafuta Buan milele, akifanya majaribio ya kumuangamiza. Hivyo inahisiwa Kupatwa kwa jua kunaelezewa na Arao kukaribia vya kutosha kumuuma. Ambapo Alfajiri Buan huficha nyota zake na huzitoa wakati binti yake mkubwa Tala nyota ya jioni na asubuhi hutokea akiamini jua liko mbali sana kuwafuata.

Kulingana na hadithi hii ni maneno ya Tagalog tala, ambayo inamaanisha "nyota mkali", araw jua na buwan mwezi.

Kutoka katika hadithi za Kapampangan, mungu anayeitwa Tálâ pia yupo anapatikana. Katika hadithi hizo za Kapampangans inaelezwa Tálâ ndiye nyota mkali na ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa utamaduni wa mpunga wa maji huko Pampanga.