Back

ⓘ Panya-vinamasi
                                     

ⓘ Panya-vinamasi

Panya-vinamasi ni wanyama wagugunaji wa jenasi Dasymys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae ambao wanatokea Afrika kusini kwa Sahara katika vinamasi na maeneo manyevu mengine yenye nyasi ndefu nyingi, mara nyingi kwenye miinuko.

                                     

1. Maelezo

Panya hao wanaonekana kuwa wenye nguvu na manyoya marefu. Wana uso bapa kiasi na masikio pinki ya mviringo. Urefu wa mwili ni sm 12-19, urefu wa mkia sm 10-18 na uzito ni g 80-165. Nyayo zao ni ndefu. Manyoya ni kahawia iliyoiva hadi meusi lakini meupe upande wa chini.

Haijulikani sana juu ya mwenendo wa panya-vinamasi kwa sababu ya ugumu wa kunasa vielelezo hai na tabia yao ya kuishi katika vikundi vidogo vilivyotengwa. Panya-vinamasi hujulikana kujenga viota tata ili kubaki wakilindwa wakati wa kunyonyesha wachanga wao. Hukiakia usiku ingawa wengine walionekana wakati wa mchana. Huishi ardhini lakini huingia maji mara nyingi na kwa kawaida huchimba vishimo vyao kando ya kingo za mito vinavyopita sambamba na mto au kuuelekea moja kwa moja. Panya-vinamasi wanaweza kuogelea vizuri na hata kuogelea kupitia vishimo vyao, wakati vimejaa maji.

Lishe ya panya-vinamasi kimsingi imeundwa na dutu ya mimea kijani. Walakini, vielelezo vingine vimeonekana na wadudu kwenye yaliyomo ndani ya tumbo pia. Lakini hula mimea hasa. Kwa kawaida hutegemea mashina na vichwa vya nyasi na matete yanayokua majini karibu na vishimo vyao.

                                     

2. Spishi

 • Dasymys alleni, Panya-vinamasi wa Allen Glover Allens shaggy rat – Tanzania
 • Dasymys cabrali Crawford-Cabrals shaggy rat
 • Dasymys nudipes Angolan marsh rat
 • Dasymys medius, Panya-vinamasi milima Montane shaggy rat – Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda
 • Dasymys robertsii Robertss shaggy rat
 • Dasymys rwandae, Panya-vinamasi wa Rwanda Rwandan shaggy rat – Rwanda
 • Dasymys longipilosus Long-haired shaggy rat
 • Dasymys shortridgei Robertss shaggy rat – labda kisawe cha D. cabrali
 • Dasymys sua, Panya-vinamasi wa Tanzania Tanzanian shaggy rat – Tanzania
 • Dasymys capensis Cape shaggy rat
 • Dasymys foxi Foxs shaggy rat
 • Dasymys griseifrons Grey-fronted shaggy rat
 • Dasymys incomtus African marsh rat
 • Dasymys montanus, Panya-vinamasi wa Ruwenzori Montane shaggy rat – Uganda
 • Dasymys rufulus, Panya-vinamasi wa Kawaida West African shaggy rat – Kenya, Tanzania, Uganda
                                     
 • India huwa na visa vingi vya malaria kutokana na hali ya hewa ya joto na vinamasi vinavyohimiliwa wakati wa kiangazi na chemichemi inayotiririka kutoka vilima

Users also searched:

...