Back

ⓘ Chinwe Chukwuogo-Roy
                                     

ⓘ Chinwe Chukwuogo-Roy

Chinwe Ifeoma Chukwuogo-Roy alikuwa msanii wa sanaa ya uchoraji aliyezaliwa nchini Nigeria katika jimbo la Anambra lakini altumia muda wake mwingi wa maisha ya ujana katika mpaka wa nchi ya Kamerun kabla ya kurejea katika makazi ya familia yake huko Umubele na mwaka 1975 alikwenda kuishi Uingereza.

Michoro yake, machapishio na michongo yake vimekuwa katika maumbo tofauti na kumfanya kuweza kuonekana zaidi kimataifa mwaka 2002 yeye pamoja na Ben Enwonwu walipata nafasi ya kufanya mchoro wa Malkia wa Elizabeth wa pili wa Uingereza.

Chukwuogo-Roy alichaguliwa kuwa mwanachama katika The Order of the British Empire MBE katika sherehe ya siku ya kuzaliwa mwaka 2009.