Back

ⓘ Magdalene Odundo
Magdalene Odundo
                                     

ⓘ Magdalene Odundo

Magdalene Anyango Namakhiya Odundo ni Mkenya aliyekuwa akiishi Franham. alikuwa mkuu wa chuo katika chuo kikuu cha Sanaa cha University for the Creative Arts tangu mwaka 2018.

                                     

1. Maisha ya Awali na Elimu

Magdalene Odundo alizaliwa katika jiji la Nairobi na kupata elimu yake katika nchi ya India na Kenya. Mwaka 1971 alihamia nchini Uingereza kwa ajili ya kujifunza zaidi kuhusu sanaa za utengenezaji wa picha baada ya kumaliza mafunzo alihamia Farnham, Surrey, Odundo ni muhitimu wa sanaa katika chuo cha sanaa cha Cambridge School of Art,ambapo alianza rasmi kuwa mtaalamu katika sanaa za utengenezaji wa bidhaa za Kauri.

Kati ya Mwaka 1974 na 1975 baada ya kukaa kwa muda katika nchi ya Uingereza, aliamua kutembelea nchini Nigeria ambako alianza kujiufnza na kufahamu zaidi kuhusiana na sanaa ya Ufinyanzi wakati alipotembelea katika kituo cha Pottery Training Centre katika jiji la Abuja, na kisha alirudi Kenya kwa ajili ya kujifunza mbinu za asili za uifnyanzi.Magdalene alipata shahada ya sanaa katika chuo cha Royal College of Art mjini London. alifunisha katika chuo cha Commonwealth Institute kuanzia mwaka 1976 hadi mwaka 1979 na chuo cha Royal College of Art kuanzia mwaka 1979 hadi 1982, kabla ya kurejea na kufundisha katika chuo cha Surrey Institute of Art & Design kwa sasa ni chuo kikuu cha University for the Creative Arts mwaka 2001 alikuwa profesa katika masuala ya sanaa.