Back

ⓘ Jamii:Miungu ya Misri ya Kale
                                               

Amun

Amun alikuwa mmoja wa miungu wakuu katika dini ya Misri ya Kale. Aliabudiwa pamoja na mke wake Ament. Ushuhuda wake Amun unapatikana tangu Himaya ya Kale ya Misri. Wakati wa nasaba ya 11 karne ya 21 KK Amun alikuwa mungu mkuu wa mji mkuu wa Thebi.

                                               

Anubis

Anubis alikuwa mmoja kati ya miungu katika dini ya Misri ya Kale. Alitazamwa kuwa mlinzi wa milango ya ahera. Awali aliabudiwa pia kama mungu aliyehusika na wafu, lakini baadaye Osiris alichukua nafasi hiyo. Anubis alionekana kama mtu mwenye kichwa cha mbweha. Imani ya Anubis ilibadilika katika historia ndefu ya Misri ya Kale. Wakati wa nasaba ya kwanza mnamo 3000 KK alitazamwa kama mlinzi wa makaburi, alitazamwa pia kuhusika na shughuli za kuandaa maiti kwa mazishi. Wakati wa Himaya ya Kati kazi yake ya kusimamia ahera ilihamishwa kwenda Osiris. Anubis alibaki na kazi ya kuongoza roho za ...

                                               

Aten

Aten ni jina la Jua lililoabudiwa kama mmoja kati ya miungu mingi nchini Misri, hasa wakati wa Farao Akhenaten. Mungu aliyeabudiwa kwa umbo la Jua nchini Misri tangu kale alikuwa Ra. Kiasili Aten alikuwa duara ya Jua tu inayoonekana angani, ikachukuliwa kama ishara ya Ra au sura yake mojawapo. Aten aliitwa mwanzoni "jicho la Ra" na baadaye "kiti cha Ra". Aten alichorwa kama duara pamoja na miale iliyoishia katika mikono. Polepole wakati ibada za Aten yenyewe zilipoanza na chini ya Farao Amenhotep III 1386 KK hadi 1349 KK Aten aliabudiwa akionyeshwa kama binadamu mwenye kichwa cha ndege koz ...

                                               

Horus

Horus alikuwa mmoja wa miungu ya Misri ya Kale. Katika mitholojia ya Kimisri alikuwa mwana wa Isis na Osiris. Aliabudiwa hasa kama mungu wa anga na pia mungu wa ufalme. Ibada yake iliendelea kwa muda mrefu, kuanzia nasaba ya kwanza hadi wakati wa Misri ya Kiroma. Katika kipindi hicho mawazo mengi kuhusu Horus yalitokea akaabudiwa kwa maumbo mengi tofauti. Lakini umbo kuu lilikuwa ndege ya kozi au mwanadamu mwenye kichwa cha kozi. Horus, aliabudiwa kote Misri, haswa huko Pe, Bendet na Khem.