Back

ⓘ Kuua kwa kukusudia
Kuua kwa kukusudia
                                     

ⓘ Kuua kwa kukusudia

Kuua kwa kukusudia ni kosa la jinai kadiri ya sheria ambapo mtu mmoja anasababisha kifo cha mtu mwingine kwa makusudi na kwa nia mbaya.

                                     

1. Katika sheria za Tanzania

Sheria ya Tanzania inafafanulia: "Mtu yeyote ambaye, kwa dhamira ya uovu, anasababisha kifo cha mtu mwingine kwa kitendo kisicho halali au kuacha kutenda ana hatia ya kuua kwa kukusudia."

Adhabu ya kuua kwa kukusudia ni adhabu ya kifo, ingawa adhabu hiyo haijatekelezwa tena Tanzania tangu mwaka 1994, nchini Kenya tangu 1987, Uganda tangu 2005.

                                     

2. Adhabu yake

Idadi ya nchi zilizofuta adhabu ya kifo inazidi kuongezeka.

Katika sheria za kisasa uuaji wa makusudi hutazamwa kama jinai dhidi ya jamii unaopaswa kuadhibiwa na dola. Katika mifumo ya sheria ya kimapokeo ulitazamwa mara nyingi kama jambo la binafsi, pia kwa kutotofautisha kati ya kuua kwa kusudi na bila kusudi; hapo ukoo wa aliyeuawa alikuwa na haki ya kulipiza kisasi kwa kumwua muuaji au ndugu wake. Ili kupakana marudio ya kisasi mifumo mingi ya kimapokeo ilijua pia malipo ya fidia.

Mfumo wa fidia unapatikana katika nchi kadhaa zinazofuata sharia ya Kiislamu ambako ni juu ya familia ya aliyeuawa kuamua kuhusu fidia au utekelezaji wa adhabu ya kifo.

                                     

3. Viungo vya Nje

  • Lord Mustill on the Common Law concerning murder
  • The Seville Statement
  • Cezannes depiction of "The Murder" – National Museums Liverpool
  • Introduction and Updated Information on the Seville Statement on Violence
  • Atlas of United States Mortality – U.S. Centers for Disease Control