Back

ⓘ NauliNauli
                                     

ⓘ Nauli

Nauli ni ada inayolipwa na abiria kwa matumizi ya chombo cha usafiri wa umma kama vile reli, basi, teksi, ndege n.k.

Muundo wa nauli ni mfumo uliowekwa kuamua ni kiasi gani kinachopaswa kulipwa na abiria anuwai wanaotumia usafiri fulani wakati wowote.

Nauli inayolipwa ni mchango kwa gharama za uendeshaji wa mfumo wa usafirishaji unaohusika, ama kisehemu jinsi ilivyo kawaida na mifumo inayoungwa mkono na umma au jumla.

Katika mifumo mingi ya usafiri abiria hukata tiketi kabla ya kuanza safari inayolipa gharama hadi kufika mwisho wa safari yake. Nauli inaweza kuwa kwa bei moja kwa matumizi ya usafiri bila kujali umbali, jinsi ilivyo kawaida katika daladala na matatu kwenye miji ya Afrika ya Mashariki", au inaweza kuwa tofauti kulingana na umbali wa safari jinsi ilivyo katika huduma za reli na za ndege.

Wakati wa kutumia usafiri wa pekee kama teksi, nauli inaamuliwa mara nyingi baada ya safari kulingana na umbali na muda wa safari.

Katika mifumo sahili kuna makondakta wanaokusanya pesa ndani ya chombo cha usafiri, mara nyingi kwa kutoka tiketi kama ushuhuda wa malipo na pia kama risiti.

Nauli za adhabu ni nauli zinazotozwa kwa abiria wasio na tiketi halali.

Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →