Back

ⓘ Lorenzo de' Medici
Lorenzo de Medici
                                     

ⓘ Lorenzo de Medici

Lorenzo de Medici alikuwa mfanyabiashara na mwanasiasa katika mji wa Firenze nchini Italia wakati wa karne ya 15. Aliitwa pia na watu wa mji wake Lorenzo il Magnifico. Lorenzo alizaliwa katika familia ya Medici waliokuwa wafanyabiashara tajiri na babu yake Cosimo de Medici aliwahi kupanda ngazi kuwa mtawala wa Firenze.

Firenze ilikuwa wakati ule dola-mji na jamhuri ya kujitegema iliyokuwa tajiri kutokana na biashara yake ya kimataifa; ilikuwa kitovu cha kiuchumi ambako benki za kwanza za Ulaya zilipoundwa. Utajiri wa mji uliwezesha taasisi za elimu na kazi ya wasanii wengi, na familia ya Medici ilikuwa kati ya wafadhili mashuhuri zaidi wa elimu na sanaa wakati wa Zama za Mwamko.

Lorenzo alitumia utajiri wake kuwa kiongozi halisi wa siasa ya Firenze ingawa hakuchaguliwa katika ofisi yoyote. Wakati wake viongozi waliochaguliwa katika halmashauri ya serikali ya jamhuri hiyo walimtegemea kifedha na kisiasa. Anajulikana zaidi kwa ufadhili wake wa wasanii mashuhuri kama vile Sandro Botticelli na Michelangelo Buonarroti. Ufadhili huo na ujenzi wa majengo mazuri kama makanisa na majumba ulikuwa sababu ya kumwita "il magnifico" mwadhimu.

Lorenzo mwenyewe alikuwa pia msanii aliyetunga mashairi. Alizaa watoto 10 na mmojawao aliyeitwa Giovanni akawa Papa Leo X.

                                     

1. Kujisomea

  • Peter Barenboim, Michoro ya Michelangelo - Ufunguo wa Tafsiri ya Medici Chapel.
  • Christopher Hibbert, Nyumba ya Medici: Kuibuka na Kuanguka kwake Morrow-Quill, 1980; historia ya jumla ya familia.
  • Miles J. Unger, Magnifico: Maisha ya kipaji na nyakati za vurugu za Lorenzo de Medici Simon na Schuster 2008, wasifu wa Lorenzo.
  • FW Kent, Lorenzo de- Medici na Sanaa ya Ukubwa The Johns Hopkins Symposia in Comparative History The Johns Hopkins University Press, 2004; muhtasari wa uhusiano wa Lorenzo na sanaa.
                                     
  • wa watawala wa Medici wa Firenze Lorenzo de Medici 1449 1492 mtawala wa Firenze aliyetumia pesa nyingi kwa sanaa Giovanni de Medici 1475 1523
  • 1513 hadi kifo chake. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Giovanni di Lorenzo de Medici Alimfuata Papa Julius II akafuatwa na Papa Adrian VI. Leo X ndiye
  • 2014 - 2015 Troy Otto katika Fear the Walking Dead 2017 na Lorenzo de Medici katika Medici The Magnificent 2018 Pia alifanywa nyota katika filamu