Back

ⓘ Klotilda malkia
Klotilda malkia
                                     

ⓘ Klotilda malkia

Klotilda malkia alikuwa mtoto wa Kilperiko II, mfalme wa Burgundy, halafu mke wa Klovis, mfalme wa Wafaranki, ambao wazao wake wakaja kutawala kwa miaka zaidi ya 200.

Tangu alipoolewa 493 alijitahidi kumvuta kwenye Ukristo hadi akafaulu kumfanya abatizwe 496. Tukio hilo likawa na matokeo makubwa kwa historia ya Kanisa na ya Ulaya nzima, kwa kuwa kabila lote lilimfuata kuingia Kanisa Katoliki bila kupitia Uario uliowahi kufuatwa na makabila mengine ya Kijerumani. Ushirikiano wa Wafaranki na Mapapa ukaanda mwanzo wa Dola Takatifu la Kirumi wakati wa Karolo Mkuu.

Baada ya kufiwa mumewe alikwenda kuishi monasterini pamoja na kusaidia maskini na kujenga makanisa.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake.

                                     
  • kumbukumbu za watakatifu Karolo Lwanga na wenzake, Sesili wa Karthago, Klotilda malkia Lifardi, Oliva wa Anagni, Isaka wa Cordoba, Davini wa Lucca, Yohane
  • Ndiyo Ndiyo Ndiyo Klinio Ndiyo Ndiyo Ndiyo Klod Ndiyo Ndiyo Klotilda malkia Ndiyo Ndiyo Ndiyo Kluthi Ndiyo Ndiyo Ndiyo Ndiyo Kointa Ndiyo