Back

ⓘ Maneno saba
Maneno saba
                                     

ⓘ Maneno saba

Maneno saba katika Ukristo ni yale ambayo Yesu aliyatamka akiwa msalabani na yamerekodiwa katika Injili nne.

Kati yake, matatu yanapatikana katika Injili ya Luka tu, mawili katika Injili ya Yohane tu. Lingine linapatikana katika Injili ya Mathayo na Injili ya Marko vilevile. Lingine tena limerekodiwa na Yohane lakini Mathayo na Marko wamelidokeza.

Katika Mathayo na Marko, Yesu Kristo anamlilia Mungu. Katika Luka, yeye anawasamehe wauaji wake, anamfariki mhalifu aliyetubu, na kumkabidhi Baba roho yake. Katika Yohane, Yesu anasema na mama yake na mwanafunzi mpendwa, anatokeza kiu yake, na kutangaza utimilifu wa kazi na maisha yake yote kadiri ya mpango wa Mungu.

Maneno ya buriani ya mtu yeyote yanatiwa maanani sana. Yanaweza kusaidia kuelewa nini ilikuwa muhimu kwake. Ilikuwa hivyo hasa kwa Yesu aliyeweza kusema machache tu kutokana na hali yake.

Tangu karne ya 16 maneno hayo yametumika sana katika mahubiri ya madhehebu mbalimbali siku ya Ijumaa kuu, na vitabu vingi vimetungwa kuyafafanua.

Watunzi mbalimbali waliyatia katika muziki.

Mpangilio wa kawaida ni huu:

 • Yoh 19:30
 • Yoh 19:26–27
 • Lk 23:46
 • Lk 23:43
 • Math 27:46 na Mk 15:34
 • Yoh 19:28
 • Lk 23:34
                                     
 • Yesu akiwa msalabani alisema maneno kadhaa. Kati ya hayo, ni maarufu maneno saba yaliyoripotiwa na Injili yakimuelekea Mungu Baba, Bikira Maria, Mtume
 • Viwakilishi vya - a unganifu ni neno maneno ya sifa - yanayosimama badala ya nomino inayosifiwa kwa kutumia mzizi wa - a unganifu. Mifano Ya moto yanaunguza
 • Kiingereza, na hoja zao kukosa mashiko. Lugha ya Kiswahili ina aina saba tu za maneno ambazo ni: Nomino N Viwakilishi W Vivumishi V Vitenzi T, Ts
 • INRI ni kifupisho cha maneno ya Kilatini Iesus Nazarenus Rex Iudaeorum Yesu Mnazareti Mfalme wa Wayahudi Ni kwamba, kadiri ya Injili zote nne, Ponsio
 • inayosherehekewa kati ya Wamarekani Weusi nchini Marekani kwa muda wa siku saba toka tarehe 26 mwezi wa disemba hadi tarehe 1 mwezi wa Januari. Sikukuu hii
 • mahali popote tunapojua au tunapoweza kutambua. Katika lugha ya kila siku maneno anga na mbingu mara nyingi yanatumiwa kwa maana moja: Mawingu yanatembea
 • mtu lazima acheze kwa mwaka ngoma yao kuu hufanyika mwezi wa saba kuanzia tarehe saba hadi kumi katika kijiji cha Chambalo. 10. wao wanaamini pombe ni
 • Ni mafumbo kwa kuwa ishara ya nje vitendo na vitu vinavyosindikizwa na maneno maalumu zinamletea mtu neema zisizoonekana. Wakatoliki wanasadiki zina
 • sarufi ni Kiarabu, lakini lugha imepokea maneno mengi kutoka Kiitalia na Kiingereza. Siku hizi takriban nusu ya maneno yana asili ya Kiitalia, na theluthi
 • Hakuna matata ni maneno ya Kiswahili yaliyopata kuwa maarufu kutokana na matumizi katika wimbo wa filamu ya Disney The Lion King. Kwa njia hiyo yalijulikana