Back

ⓘ Ukatili
Ukatili
                                     

ⓘ Ukatili

Ukatili ni hali ya kusababisha kwa makusudi mateso na kukosesha raha dhidi ya mtu mwingine, ilihali suluhisho la wazi linapatikana kwa urahisi.

Ukatili unaweza kutokana na matatizo ya kisaikolojia yenye mizizi utotoni, lakini pia ni tabia ambayo mtu anaweza kujijengea kinyume cha maadili.

Ukatili unaweza kujitokeza hata katika namna ya kufanya ngono.

                                     

1. Matumizi katika sheria

Neno ukatili mara nyingi hutumika katika sheria kuhusu matendo dhidi ya watoto, wenzi wa ndoa, na wafungwa lakini pia dhidi ya wanyama. Ukatili kwa wanyama unapojadiliwa, mara nyingi humaanisha mateso yasiyofaa, yaani yasiyo na sababu ya kutosha, si yale yanayotakiwa na ulaji wa nyama yake.

Katika sheria ya jinai, inamaanisha mateso, unyanyasaji na adhabu kali na isiyo ya kawaida. Katika visa vya talaka, mamlaka nyingi huiruhusu kwa ajili ya matendo ya kikatili na ya kinyama. Katika sheria, ukatili ni "usumbufu wa kimwili au kiakili, haswa inapofikiriwa kwa uamuzi wa kutoa talaka."

                                     

2. Marejeo

  • Susan Sontag, Regarding the Pain of Others, 2003.
  • Simon Baron-Cohen, The Science of Evil: On Empathy and the Origins of Cruelty, Basic Books, 2011. Reviewed in The Montreal Review