Back

ⓘ Azimio la kazi
                                     

ⓘ Azimio la kazi

Azimio la kazi ni mpango kazi unaoandaliwa na mwalimu ambao unaonesha mpangilio wa kufundisha mada mbalimbali kwa kipindi maalumu katika muhtasari wa somo husika. Huo ni mpango wa ufundishaji kwa kipindi fulani ambao kila mwalimu anauandaa ili kukidhi lengo la ufundishaji.

Mwalimu anaweza kuandaa azimio la kazi katika kipindi cha wiki, mwezi, nusu muhula au muhula mzima. Kitendo hiki cha uandaaji, kinaweza kumsaidia mwalimu kulipanga darasa lake vizuri na hata kujua vifaa atakavyovitumia wakati wa ufundishaji wake.

                                     

1. Umuhimu wa Azimio la kazi

- Kumsaidia mwalimu kwenda na mpangilio mzuri wa mada.

- Humsaidia mwalimu wapi alipofikia na kumfanya mwalimu anayempokea somo lake kujua wapi alipoishia.

- Kujua muda wa kumaliza mada yake/zake.

- Kumwezesha mwalimu kujua zana atakazozitumia katika ufundishaji wake.

                                     

2. Vipengele muhimu vilivyomo katika Azimio la kazi

i) Muhula: Sehemu hii huandikwa namba ya muhula ambapo Azimio la kazi litatumika.

ii) Mwezi: Sehemu hii huandikwa jina la mwezi ambao mada fulani zitafundishwa.

iii) Ujuzi: Haya ni maarifa,stadi ambayo mwanafunzi hupata baada ya kufundishwa.

iv) Wiki: Sehemu hii huandikwa idadi ya wiki katika mwezi ambapo somo hilo litafundishwa.

v) Idadi ya vipindi: Hapa huandikwa idadi ya vipindi katika juma au majuma yaliyooneshwa.

vi) Mada kuu: Sehemu hii huandikwa mada kuu itakayofundishwa katika kipindi hicho.

vii) Mada ndogo: Sehemu hii huandikwa mada ndogo itakayofundishwa.

viii) Vitendo vya ufundishaji: Sehemu hii hujazwa na mwalimu kounesha harakati zake za kuwapa somo husika wanafunzi.

ix) Vitendo vya ujifunzaji: sehemu hii huandikwa harakati za wanafunzi wakati wa kupokea somo.

x) Vifaa/zana: Katika sehemu hii, mwalimu huandika vifaa au zana atakazozitumia wakati wa ufundishaji wake.

xi) Rejea: Sehemu hii mwalimu ataandika vitabu alivyovitumia katika ufundishaji wake.

xii) Maoni: Katika sehemu hii mwalimu atatoa maoni yake kuhusu mafanikio, changamoto alizozipata katika ufundishaji wake na njia atakazozitumia katika kuboresha zaidi ufundishaji wake.

                                     
  • Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu pia: Tangazo la kilimwengu la haki za binadamu au Taarifa ya Ulimwengu juu ya Haki za Binadamu, kwa Kiingereza:
  • kwa azimio ya kamati au mahakama ya kimataifa nchi wanachama zote zitaungana dhidi ya nchi yoyote itakayoanzisha vita mpya au kukataa azimio la mahakama
  • kuzuia habari juu ya matendo yao. Ingawa nchi karibu zote zimekubali Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu ambamo Kifungu cha 19 inasema Kila
  • kolonia zao zilizoendelea kutumia kazi ya watumwa katika uchumi wa mashamba ya miwa na mazao mengine. Lakini azimio la Vienna ilikuwa hatua muhimu katika
  • 1933 na 1945. Siku hiyo iliteuliwa kwa azimio la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa 60 7 mnamo 1 Novemba 2005. Azimio hilo linasema haswa: Kuthibitisha kwamba
  • zilizoanzishwa tayari: Afrika Kusini ilikataa azimio la mwaka 1971 la kujiondoa katika Namibia Ufaransa ilikataa 1973 azimio la kusimamisha majaribio na mabomu ya
  • aliitisha Bunge la Uingereza akawalazimisha wabunge kutangaza kwamba mfalme ndiye mkuu wa kanisa nchini. Halafu bunge lilikubali talaka yake. Azimio lingine lilikuwa
  • lugha tofauti. Azimio la kutangaza mwaka huo linataja pia shida za lugha ndani ya Umoja wa Mataifa wenyewe. Shirika la UNESCO limepewa kazi ya kupanga utekelezaji
  • 1967 Rais Nyerere alichapisha mwongozo wa maendeleo yake, ambao uliitwa Azimio la Arusha, ambapo alionyesha haja ya kuwa na mtindo wa Kiafrika wa maendeleo