Back

ⓘ Kardinali mlinzi
Kardinali mlinzi
                                     

ⓘ Kardinali mlinzi

Kardinali mlinzi alikuwa kardinali aliyeteuliwa na nchi, mashirika ya kitawa, vyama vya kitume, makanisa, mabweni na miji au aliyetolewa na Papa kwa miundo hiyo ili aisimamie kwa niaba yake na kuitetea huko Roma katika ofisi kuu za Kanisa Katoliki.

Desturi hiyo ilianza katika karne ya 13 Fransisko wa Assisi alipomuomba papa Inosenti III na halafu papa Onori III apewe Ugolino, kardinali wa Ostia, kama mlinzi wa utawa wake wa Ndugu Wadogo.

Mamlaka ya kardinali mlinzi iliongezwa au kupunguzwa kadiri ya mangamuzi mpaka iliposimamishwa kwa jumla baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano 1962-1965.