Back

ⓘ Lanthanidi
                                     

ⓘ Lanthanidi

Lanthanidi ni kundi la elementi za kimetali zenye namba atomia kutoka 57 hadi 71, ambazo tabia zake zinafanana. Elementi hizo huhesabiwa kati ya madini adimu kama vile monaziti. Kundi hilo huanza na lanthani na kuishia kwa luteti.

Lanthanidi ni metali zinazofanana katika tabia nyingi. Nyingi hubadilika polepole kuwa hidroksidi zake wakati zimewekwa ndani ya maji, sawa na metali alikali.

Hewani huunda kwa kawaida ganda jembamba la oksidi wakati sawa na metali nyingi. Lanthanidi, pamoja na Skandi na Ytri, huhesabiwa kati ya elementi za ardhi adimu. Lanthanidi zote ni metali nyeupe na laini zinazobadilisha rangi ya nje haraka zikiathiriana na hewa. Ugumu wake huongezeka sambamba na namba atomia.

Lanthanidi hazipatikani wala hazichimbwi kwa viwango vikubwa.

                                     

1. Matumizi

Zina matumizi katika teknolojia mbalimbali kama vile:

* Ceri: hutumiwa kama "jiwe la kibiriti" katika vibiriti vya gesi; pia kama kichocheo katika pirolisisi

* Disprosi: hutumiwa kufyonza nyutroni ndani ya tanuri nyuklia

* Erbi: imo katika filta za kupiga picha

* Europi: hutumiwa kufyonza nyutroni ndani ya tanuri nyuklia, lakini pia kwa kuwasha rangi nyekundu katika skrini ya runinga

* Gadolini: hutumiwa kuwasha rangi kibichi katika skrini ya runinga

* Holmi: hutumiwa katika aloi; kwa jumla lanthanidi mbalimbali hutumiwa kama sehemu za aloi maana zinasaidia feleji kuwa nyumbufu zaidi wakati wa kuipa umbo

* Luteti: kichocheo katika pirolisisi

* Neodimi: huhitajika kwa sumaku kali; pia sehemu ya vioo vya miwani ya kinga cha mtia weko, hutumwa pia katika leza.

* Praseodimi: katika kioo njano, k.v. kwa miwani ya kinga cha mtia weko.

* Promethi: ikiwa ni nururifu hutumiwa kama chanzo cha nishati kwa satelaiti na vipimaanga

* Samari: kama sumaku ya kudumu, mfano katika kipaza sauti

* Terbi: kwa leza

* Thuli: kufyonza nyutroni ndani ya tanuri nyuklia

* Yterbi: hutoa eksirei ilhali haihitaji umeme, mfano katika mashine za eksirei za kubeba

                                     

2. Viungo vya nje

 • Ana de Bettencourt-Dias: Chemistry of the lanthanides and lanthanide-containing materials
 • lanthanide Sparkle Model, used in the computational chemistry of lanthanide complexes
 • Eric Scerri, 2007, The periodic table: Its story and its significance, Oxford University Press, New York, ISBN 9780195305739
 • USGS Rare Earths Statistics and Information
                                     
 • imepangwa katika kundi la metali za mpito na kati ya lanthanidi Tabia zake hulingana na lanthanidi kwa jumla. Iligunduliwa mwaka 1907 na wanakemia mbalimbali
 • rangi ya kifedha - kijivu, chumvi zake ni njano - kijani. Huhesabiwa kati ya Lanthanidi na metali za ardhi adimu. Inachanganywa na magnesi kutengeneza aloi thabiti
 • katika atomu. Europi imepangwa kwenye jedwali la elementi katika kundi la lanthanidi Ni elementi inayotendana haraka sana na hewa au unyevu, hivyo inahitaji
 • Uzani atomia ni 147. Ndani ya jedwali la elementi imepangwa kati ya lanthanidi Isotopu zake zote ni nururifu. Promethi na Tekineti ndizo elementi mbili
 • elements, rare earth metals ni jumla ya elementi 17 za kikemia zikiwa lanthanidi 15 pamoja na Skandi na Ytri. Skandi na Ytri zinahesabiwa kati ya ardhi
 • na uzani atomia 162.50. Alama yake ni Dy. Disprosi huhesabiwa kati ya Lanthanidi inaonekana kama metali nzitonzito yenye rangi ya kifedha. Haina matumizi
 • kikemia katika mfumo radidia Metali alikali Metali za udongo alikalini Lanthanidi Aktinide Metali mpito Metali Metaloidi Simetali Halojeni Gesi adimu Mfumo
 • Uzani atomia ni 140.12. Ndani ya jedwali la elementi imepangwa kati ya lanthanidi Seri ni metali yenye rangi ya kijivu. Kwa joto la kawaida inapatikana