Back

ⓘ Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini
                                     

ⓘ Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini

Maisha Yangu Baada ya Miaka Hamsini ni kitabu kilichoandikwa na Shaaban Robert mwenyewe akielezea historia na matukio yaliyotokea katika maisha yake na changamoto mbalimbali alizozipitia katika maisha yake ya kikazi kama muajiriwa wa Serikali na baadae kama muandishi wa mashairi.

Kitabu hiki kitawasaidia sana wasomi, wataalamu na waandishi wa fasihi ya Kiswahili katika kufanya utafiti wa masuala mbalimbali yanayohusu fasihi kwa ujumla na wanafasihi wake.

Ndani ya kitabu hiki zinapatikana zile tenzi mbili maarufu za Utenzi wa Hati na Adili ambazo aliwaandikia watoto wake wawili Mwanjaa na Suleyman

Japokuwa ametumia lugha ya kifasihi sana katika kitabu hiki, lakini Shaaban Robert ameweza kueleza mambo mbalimbali aliyowahi yapitia kama vile ubaguzi wa rangi aliowahi fanyiwa wakati anasafiri kikazi ndani ya Tanganyika wakati wa ukoloni tukio ambalo lilitokea 13 Julai 1944 wakati anatoka Korogwe, mkoa wa Tanga, kuelekea Mpwapwa.