Back

ⓘ Lviv
Lviv
                                     

ⓘ Lviv

Lviv ni makao makuu ya Lviv Oblast nchini Ukraine. Jiji hilo lina wakazi 860.000, ilhali asilimia 88 ya watu wanaoishi huko ni Waukraine asilia, % 8 ni Warusi, na % 1 ni Wapoland.

                                     

1. Historia

Katika historia yake, jiji hilo lilikuwa sehemu ya milki na nchi mbalimbali. Liko mahali ambako tamaduni za Poland na Ukraine zinakutana. Kwa muda mrefu lilikuwa mji wa Kipoland kwa jina la "Lvov" wenye wakazi wengi kiasi wa Kiyahudi, ilhali Waukraine waliishi katika maeneo ya vijijini ya mazingira ya mji. Hadi mwaka 1772 ilikuwa sehemu ya milki ya Poland.

Wakati wa kugawiwa kwa Poland sehemu hii iliwekwa chini ya utawala wa Austria ulioleta Wajerumani, hasa watumishi wa serikali, kuhamia Lvov. Serikali ya Austria ilitumia jina la Kijerumani "Lemberg".

Mwaka 1918 utawala wa Austria ulikwisha na Lvov ilikuwa tena mji wa Poland. Wayahudi walikuwa takriban theluthi moja ya wakazi.

Mwaka 1939 Poland ilishambuliwa na Ujerumani, na Jeshi Jekundu la Umoja wa Kisovyeti iliteka mashariki ya Poland, pamoja na Lvov.

Mwaka 1941 Ujerumani ilishambulia Umoja wa Kisovyeti na kuteka Lvov hadi 1944. Wajerumani walianza mara moja kukusanya Wayahudi na kuwaua. Wayahudi wachache tu waliishi kuona mwisho wa vita na uhuru mpya.

Mwaka 1944 jeshi la Kisovyeti lilirudi mjini, na tangu mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia 1945 mji ulikuwa sehemu ya Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiukraine kwa jina la Kiukraine "Lviv". Hii ilifanya Wapoland wengi kuondoka mjini na kuhamia Poland yenyewe.

Tangu kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti Lviv ni mji wa nchi huru ya Ukraine. Wakazi wengi kabisa ni Waukraine.

Leo hii Lviv ni mji unaovuta watalii wengi ambao wanapenda kutembelea kitovu cha kihistoria cha mji chenye majengo mengi ya zamani za Milki ya Austria ambayo yametengenezwa na kukarabatiwa vizuri.

                                     
  • Josef Bilczewski 26 Aprili 1860 20 Machi 1923 alikuwa askofu mkuu wa Lviv leo nchini Ukraina kuanzia mwaka 1900 hadi kifo chake. Bilczewski alisaidia
  • Polandi Yohane alizaliwa Dukla, Polandi, mwaka 1414 akafariki mwaka 1484 huko Lviv leo nchini Ukraina. Ingawa alijiunga kwanza na Ndugu Wadogo Wakonventuali
  •  Iraq Jimbo kuu la Konstantinopoli la Waarmenia Uturuki Jimbo kuu la Lviv la Waarmenia Ukraine Jimbo la Bibi Yetu wa Nareg jijiji New York Marekani
  • Donetsk International Airport Kiev - Boryspil International Airport Lviv - Lviv International Airport Ulaya Birmingham - Birmingham International Airport