Back

ⓘ Kreyol Ayisien
Kreyol Ayisien
                                     

ⓘ Kreyol Ayisien

Kreyol Ayisien au Krioli ya Haiti ni lugha ya Krioli iliyozaliwa nchini Haiti na kuwa moja ya lugha rasmi katika nchi hiyo. Ndiyo Krioli kubwa zaidi duniani kwa kuwa lugha hiyo inaongelewa na watu milioni 10-12.

Asili ya lugha ni kukutana kwa watumwa kutoka nchi za Afrika na mabwana wao waliosema Kifaransa huko Haiti.

Kifaransa na Krioli ya Haiti zinafanana sana katika msamiati; takriban asilimia 90 za maneno ya Krioli zimepokewa kutoka Kifaransa. Lakini mara nyingi maana ya maneno imebadilika, na kwa msemaji wa Kifaransa cha Kisasa si rahisi kuelewa Krioli hiyo moja kwa moja. Vilevile Kifaransa ni lugha ya pili kwa wazawa wengi wa Haiti.

Kwa miaka mingi Kifaransa sanifu kilikuwa lugha rasmi pekee lakini katiba ya mwaka 1987 ilitambua Kikrioli kama lugha rasmi ya pili.