Back

ⓘ Mchezaji bora wa mwaka wa FIFA
Mchezaji bora wa mwaka wa FIFA
                                     

ⓘ Mchezaji bora wa mwaka wa FIFA

Mchezaji bora wa mwaka ilikuwa tuzo iliyotolewa kila mwaka na mamlaka husika ya mchezo wa mpira wa miguu, FIFA kwa mchezaji bora duniani kati ya miaka 1991 na 2015. Makocha na manahodha wa timu za kimataifa na wawakilishi wa vyombo vya habari walichagua mchezaji waliodhani alionyesha kiwango bora kwa mwaka uliopita.

Mwanzoni tuzo moja ya mchezaji bora wa kiume wa mwaka ulimwenguni, sambamba kwa wanaume na wanawake zilitolewa kati ya 2001–2009. Tuzo ya wanaume ilibadilishwa kuwa Ballon dOr ya FIFA mnamo 2010 wakati tuzo za wanawake zilibakia hivyo mpaka 2015. Baada ya 2015 tuzo zote za wanaume na wanawake zilikuwa sehemu ya Tuzo bora za FIFA za mpira wa miguu.

Wakati wa enzi ya tuzo za wanaume, wachezaji wa Brazil walishinda mara 8 ndani ya miaka 19, ukilinganisha na ushindi mara tatu – kwa mara mbili – kwa wachezaji wa Ufaransa. Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja, Brazil iliongoza tena kwa ushindi wa tuzo mara tano, wakifauatiwa na Italia na Ureno walioshinda mara mbili kila mmoja. Mshindi mdogo Zaidi alikuwa Ronaldo, alishinda tuzo akiwa na miaka 20 mnamo 1996, na mshindi mkongwe Zaidi alikua Fabio Cannavaro, aliyeshinda akiwa na miaka 33 mnamo. Ronaldo na Zinedine Zidane kila mmoja ameshinda tuzo mara tatu, wakati Ronaldo na Ronaldinho" ndio wachezaji pekee walioshinda tuzo kwa miaka mfululizo. Kuanzia 2010 mpaka 2015, tuzo sawa kwa wanaume ilikuwa FIFA Ballon dOr, kufuatia kuungana kwa tuzo ya FIFA mchezaji bora wa mwaka duniani na France Football Ballon dOr. Tokea 2016, tuzo hizo zilibadilishwa na kuwa Best FIFA Mens Player na Best FIFA Wanawakes Player.

Wachezaji nane wa kike – watatu wa Ujerumani, wa tatu wa Marekani, mmoja wa Brazil, na mmoja wa japan– wameshinda tuzo hiyo. Marta, mpokeaji mdogo wa kike katika umri wa miaka 20 mnamo 2006, Ameshinda mara tano mfululizo tuzo hizo, na mara nyingi Zaidi kuliko mchezaji mwingine. Birgit Prinz ameshinda mara tatu mfululizo na Mia Hamm ameshinda mara mbili mfululizo. Mshindi mkongwe Zaidi ni Nadine Angerer, aliyekuwa na miaka 35 aliposhinda tuzo hiyo; ndiye pekee mlinda mlango kwa jinsia zote kuwahi kushinda tuzo hiyo.

                                     

1. Upigaji kura na mchakato wa uchaguzi

Washindi huchaguliwa na makocha na manahodha wa timu za taifa pamoja na wawakilishi wa vyombo vya habari vya kimataifa walioalikwa na FIFA. Kwenye mfumo wa kupiga kura uliyo katika missing ya positional voting, kila mpiga kura hugawiwa kura tatu, zenye thamani ya alama tano, alama tatu na alama moja, na tatu bora hupangwa kulingana na idadi ya alama. Kufuatia ukosoaji kutoka sehemu ya vyombo vya habari juu ya uteuzi katika miaka iliyopita, FIFA ilianza kutoa majina ya walioteuliwa kwa ajili ya kupigiwa kura kuanzia 2004.

                                     

2. Mchezaji bora wa mwaka Ulimwenguni

Source:

Kutokea 2010 mpaka 2015, tuzo iliunganishwa na Ballon dOr ili kuwa Ballon dOr ya FIFA ndani ya ushirikiano wa miaka sita na Shirikisho la mpira wa miguu Ufaransa. Mwaka 2016, FIFA ilibadili tuzo hizo kuwa Mchezaji bora wa kiume wa FIFA.