Back

ⓘ Mabasi ya mwendokasiMabasi ya mwendokasi
                                     

ⓘ Mabasi ya mwendokasi

Mabasi ya mwendokasi ni mfumo wa usafiri wa mjini ambako kuna njia za pekee za mabasi kwenye barabara zinazofungwa kwa magari madogo, mabasi ya kawaida na baisikeli. Katika mfumo huu mabasi ya mwendokasi hupewa kipaumbele kwenye njiapanda. Kuna pia mbinu za kuwezesha abiria kuingia na kuondoka pamoja na kukata tiketi haraka.

Kwa njia hiyo uwezo wa mabasi ya kubeba abiria wengi huongezwa na kuepukana na matatizo ya mabasi ya mjini ya kawaida ambayo yanaweza kukwama katika msongamano wa magari.

Kwa njia hiyo mfumo wa mabasi ya mwendokasi ina faida zinazopatikana vinginevyo kwa mfumo wa metro usafiri kwenye njia za reli au tramu usafiri kwa reli ndogo mjini lakini kwa kuepukana na gharama kubwa kutengeneza njia za reli juu au chini ya ardhi. Hata hivyo mifumo ya mabasi ya mwendokasi haifikii uwezo wa metro wa kusafirisha abiria wengi kwa wakati mfupi.

Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →