Back

ⓘ Shirika la ndegeShirika la ndege
                                     

ⓘ Shirika la ndege

Shirika la ndege ni kampuni inayotoa huduma ya usafiri wa anga wa kiraia kwa abiria na mizigo. Mashirika ya ndege hutumia ndege kutoa huduma hizi. Kawaida, mashirika haya hupewa leseni na idara husika ya serikali.

Mashirika ya ndege hutofautiana kwa ukubwa, toka mashirika ya ndege madogo ya safari za ndani na mashirika makubwa ya safari za kimataifa. Mnamo 2019 shirika la ndege kubwa kuliko yote duniani ni American Airlines Group.

                                     

1.1. Historia Mashirika ya ndege ya kwanza

DELAG, Deutsche Luftschiffahrts-Aktiengesellschaft I ndilo shirika la ndege la kwanza. Lilianzishwa Novemba 16, 1909 kwa msaada wa serikali na kumiliki ndege zilizotengenezwa na Zeppelin Corporation. Makao yake makuu yalikuwa Frankfurt.

Safari ya kwanza ya ndege ilikuwa Januari 1, 1914, toka St. Petersburg, Florida kwenda Tampa, Florida, kwa ndege iliyomilikiwa na St. Petersburg and Tampa Airboat Line.

Mashirika ya ndege ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu zaidi ni KLM 1919, Avianca 1919, Qantas 1921, na Czech Airlines 1923.

                                     

1.2. Historia Mwanzoni

Shirika la ndege zenye mabawa yasiyozunguka la mwanzo huko Ulaya ni Aircraft Transport and Travel, lililoanzishwa na George Holt Thomas mwaka 1916. Shirika la Ndege la Uingereza linatokana na shirika hili. Shirika hili lilitumia ndege zilizokuwa za kijeshi na kuzibadilisha ili ziweze kubeba abiria.

Agosti 25, 1919, shirika lilitumia ndege aina ya DH.16s kwa safari za ndege toka Hounslow Heath Aerodrome kwenda Le Bourget. Shirika hili lilipata sifa kubwa pamoja na matatizo ya hali ya hewa. Novemba 1919, shirika hili lilipata mkataba wa kusafirisha barua nchini Uingereza. Ndege sita za Jeshi la Anga la Uingereza aina ya Airco DH.9A zilitumiwa na shirika hili kusafirisha barua kati ya Hawkinge na Cologne. Mwaka 1920, ndege hizi zilirudishwa kwa jeshi hilo.

Mashirika mengine ya ndege nchini Uingereza yalifuata – Handley Page Transport liliundwa mwaka 1919 likitumia ndege aina ya Type O/400 yenye kubeba abiria 12, kwa safari za London-Paris.

Shirika la kwanza la ndege la Ufaransa lilikuwa ni Société des lignes Latécoère, baadaye liliitwa Aéropostale, ambalo lilianza kazi mwaka 1918 kwa safari za kwenda Hispania. Société Générale des Transports Aériens liliundwa mwishoni mwa 1919, na wana ndugu wa Farman na ndege ya Farman F.60 Goliath ilisafirisha watu kati ya Toussus-le-Noble na Kenley, karibu na Croydon, Uingereza. Kampuni nyingine nchini Ufaransa ilikuwa ni Compagnie des Messageries Aériennes, iliyoundwa mwaka 1919 na Louis-Charles Breguet, ikisafirisha barua na mizigo kati ya Uwanja wa Ndege wa Le Bourget, Paris na Uwanja wa Ndege wa Lesquin, Lille.

Shirika la ndege la Ujerumani la Deutsche Luft-Reederei liliundwa mwaka 1917 na kuanza kazi Februari 1919. Shirika lingine la Ujerumani lilikuwa ni Junkers Luftverkehr, lililoanza kazi mwaka 1921. Liliendesha ubia wa mashirika ya ndege nchini Austria, Denmaki, Estonia, Ufini, Hungaria, Latvia, Norway, Poland, Uswidi na Uswisi.

Shirika la ndege la Uholanzi KLM lilifanya safari ya kwanza ya ndege mwaka 1920, na ndio shirika zee kabisa duniani. Shirika hili liliundwa na Albert Plesman, Safari yake ya kwanza ilikuwa ni kutoka Uwanja wa Ndege wa Croydon, London kwenda Amsterdam.

Huko Ufini, shirika la Aero O/Y hivi sasa Finnair liliundwa huko Helsinki Septemba 12, 1923. Safari yake ya kwanza ilikuwa ni kati ya Helsinki na Tallinn, mji mkuu waEstonia, Machi 20, 1924.

Muungano wa Kisovyeti uliunda Chief Administration of the Civil Air Fleet mwaka 1921. Huduma za safari za ndani za ndege zilianza Julai 15, 1923 kati ya Moscow na Nizhni Novgorod. Toka mwaka 1932 shirika hili limekuwa likitumia jina la Aeroflot.

                                     

2. Kusoma zaidi

  • "Flying Off Course: The Economics of International Airlines," 3rd edition. Rigas Doganis, Routledge, New York, 2002.
  • "The airline encyclopedia, 1909–2000.” Myron J. Smith, Scarecrow Press, 2002
  • "A history of the worlds airlines", R.E.G. Davies, Oxford U.P, 1964
  • "The Airline Business in the 21st Century." Rigas Doganis, Routledge, New York, 2001.
                                     

3. Viungo vya nje

  • Jinsi ya kutoa malalamiko kuhusu huduma za mashirika ya ndege
  • Airline industry. Encyclopedia.com 2005.
  • Chasing the Sun. PBS." "History of commercial aviation"”
  • Global Aviation Markets - Analysis. Zinnov LLC Jan 2007.
  • Airline Cost Performance. IATA July 2006. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-02-26. Iliwekwa mnamo 2019-06-29.
Free and no ads
no need to download or install

Pino - logical board game which is based on tactics and strategy. In general this is a remix of chess, checkers and corners. The game develops imagination, concentration, teaches how to solve tasks, plan their own actions and of course to think logically. It does not matter how much pieces you have, the main thing is how they are placement!

online intellectual game →