Back

ⓘ Mabilionea Ulimwenguni
                                     

ⓘ Mabilionea Ulimwenguni

Mabilionea Ulimwenguni ni orodha ya kila mwaka ya thamani ya utajiri ya mabilionea wakubwa duniani inayoandaliwa na kuchapishwa mwezi Machi kila mwaka na gazeti la Forbes la Marekani. Orodha ya kwanza ilichapishwa Machi 1987. Jumla ya thamani ya utajiri wa kila mmoja kwenye orodha hiyo unakadiriwa na kutolewa kwa dola ya Marekani kutegemeana na mali zao na madeni. Familia za Kifalme au madikteta ambao utajiri wao unatokana na nafasi zao na sio jasho huwa hawawekwi kwnye orodha hii.

Mwaka 2018, watu 2.208 wametokea kwenye orodha hii, ambayo ilijumuisha mabilionea wapya 259 wengi wao wakitokea China na Marekani, na watu 63 wenye umri chini ya 40 na wanawake 256.

Hadi 2018, mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates alikuwa ndio namba moja kwenye orodha hii kwa miaka 18 kati ya miaka 24, wakati mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos ameshika nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza na tajiri wa kwanza kwenye orodha mwenye utajiri thamani ya dola bilioni 100. Mark Zuckerberg ni mtu pekee kwenye orodha ya mabilionea wakubwa 10 duniani mwenye umri wa chini ya miaka 50.

                                     

1. Orodha ya kila mwaka

Orodha huchapishwa kila mwaka mwezi Machi. Orodha hizi zinaonyesha mabilionea wakubwa 10 tu kila mwaka.

2019

Kwenye orodha ya Forbes ya 33, kuna mabilionea 2.153 ambao kwa ujumla wana thamani ya dola za Kimarekani trilioni 8.7.