Back

ⓘ Askofu
                                               

Mona

Monasi alikuwa askofu wa 15 wa "Milano, Italia Kaskazini. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Machi.

                                               

Zosimo wa Sirakusa

Zosimo wa Sirakusa alikuwa mmonaki wa Siracusa, Sicilia, Italia, ambaye alitazamwa kama mtu asiyeweza kitu, kumbe askofu alimfanya abati wa monasteri, halafu waumini walimchagua kuwa askofu wao. Aliongoza jimbo hilo miaka 647-662. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Machi.

                                               

Venansi, Anastasi na wenzao

Venansi, Anastasi na wenzao Mauro, Pauliniani, Telio, Asteri, Septimi, Antiokiani na Gaiani walikuwa Wakristo waliouawa katika dhuluma ya Dola la Roma kwa sababu ya imani yao. Venansi alikuwa askofu wa Salona. Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini. Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 1 Aprili.

                                               

Regulo wa Senlis

Regulo wa Senlis alikuwa askofu wa kwanza wa Senlis. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Machi.

                                               

Selso wa Armagh

Selso wa Armagh alikuwa askofu mkuu wa Armagh na Ireland yote, wakati Ukristo katika kisiwa hicho ulikuwa umepoa. Alipochaguliwa kuwa askofu ingawa bado mlei, kama ilivyomtokea babu yake, alichangia sana urekebisho wa Kanisa la huko katika karne ya 12 na kupatanisha watawala. Bernardo wa Clairvaux alimsifu kama mtu mwema na mcha Mungu. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Aprili.

                                               

Marko wa Aretusa

Marko wa Aretusa alikuwa askofu wa mji huo tangu mwaka 341 au kabla ya hapo. Aliteswa sana katika dhuluma ya kaisari Juliani Mwasi. Gregori wa Nazianzo alimsifu kama "mtu wa pekee na mzee mtakatifu sana". Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Machi.

Askofu
                                     

ⓘ Askofu

Neno episkopos linaonekana kama cheo katika maandishi ya mwisho wa karne I na mwanzo wa karne II kama vile waraka wa kwanza wa Klementi ambapo askofu aonekana kuwa kiongozi mkuu wa kanisa la mji fulani.

Katika uenezi wa Ukristo madaraka ya askofu yalipanuka. Kadiri makanisa yalivyoenea hata nje ya miji hadi mashambani askofu akawa kiongozi wa eneo, si wa mji tu.

Wakati ule ngazi za daraja zilionekana: Kanisa la mji au eneo likiongozwa na episkopos askofu akishauriana na "presbiteri" kiasili: wazee; baadaye: makasisi na kusaidiwa na mashemasi au madikoni.

                                     

1. Kanisa Katoliki na Waorthodoksi

Wakatoliki na Waorthodoksi wana daraja takatifu ya Askofu, ambaye kwa kawaida ni mkuu wa kanisa katika ngazi ya dayosisi. Askofu ni kama baba wa makasisi mapadri na waumini wengine katika eneo lake.

Maaskofu hukutana kwenye sinodi na kufanya maazimio kuhusu mambo ya Kanisa lote.

Maaskofu wa nchi au eneo kubwa wako pamoja chini ya usimamizi wa Patriarki au wa Askofu mkuu.

Katika Kanisa Katoliki askofu wa Roma ni mkuu wa Maaskofu wote na wa Kanisa lote duniani akitajwa kwa jina la Papa.

                                     

1.1. Kanisa Katoliki na Waorthodoksi Mafundisho ya mlolongo wa mitume

Katika mapokeo hayo askofu hutazamwa kama mwandamizi wa Mitume wa Yesu. Katika mafundisho hayo Yesu Kristo mwenyewe aliwaweka mitume wake 12 kuwa viongozi wa Kanisa lote na kuwapa madaraka. Madaraka hayo yalitolewa na mitume kwa kuwawekea mikono kichwani waandamizi wao waliopata hivyo kuwa maaskofu wa kwanza baada yao, nao wakafanya hivyo kwa waandamizi wao.

Kwa namna hiyo kuna mlolongo wa kuwekeana mikono kati ya wanaopokea nafasi ya uaskofu kuanzia mitume na kila kizazi cha maaskofu hadi leo. Hivyo maaskofu ni kiungo kati ya Yesu na waumini wa leo.

                                     

2. Askofu kati ya Waprotestanti

Baadhi ya madhehebu ya Uprotestanti, hasa ya Anglikana, Wamoravian na sehemu za Walutheri yanadai kuwa yameendeleza mlolongo wa mitume. Hiyo iliweza kutokea hasa katika nchi kama Uingereza na Uswidi ambako wakati wa matengenezo ya Kiprotestanti maaskofu Wakatoliki wa awali walihamia upande wa matengenezo na utaratibu wa kiaskofu uliweza kuendelea.

Pamoja na hayo, Kanisa Katoliki halikubali kwamba ilitokea hivyo kihistoria, au kwamba mtazamo wa Waprotestanti wa wakati huo kuhusu daraja takatifu na ekaristi ulitosha kushirikisha kweli mamlaka ya Mitume wa Yesu. Hivyo Kanisa hilo kwa jumla halitambui maaskofu wa Kiprotestanti kuwa na sakramenti ya daraja.

Upande wao, Waprotestanti wengi hawaoni umuhimu wa mlolongo wa kuwekewa mikono tangu wakati wa Mitume hadi leo: kwao muhimu zaidi ni uaminifu kwa imani ya Mitume.

Madhehebu mengine kadhaa ya Kiprotestanti yanatumika cheo cha askofu kuwa kiongozi katika Kanisa.

Kwa kawaida mamlaka yake ni ndogo kuliko ile ya maaskofu wa Kikatoliki na wa Kiorthodoksi, kutokana na mtazamo tofauti kuhusu Kanisa na sakramenti, ambao katika miaka ya mwisho imezidi kuwa tofauti kutokana na Waprotestanti wengi kukubali wanawake wapewe uaskofu na ukasisi, kinyume cha mapokeo na imani ya Wakatoliki na Waorthodoksi.

                                               

Anastasi wa Pavia

Anastasi wa Pavia anakumbukwa kama askofu wa 17 wa mji huo wa Italia Kaskazini kuanzia mwaka 668 hivi hadi kifo chake. Kabla ya hapo alikuwa askofu wa Pavia upande wa Waario, lakini alikanusha uzushi akashika kwa uimara imani ya Kikatoliki akipinga pia uzushi mpya kuhusu utashi wa Yesu Kristo. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Mei.

Viro
                                               

Viro

Viro alikuwa mmonaki askofu kutoka Ireland au Britania, maarufu kwa umisionari wake kati ya Wafrisia. Pamoja na wenzake Plekelmi askofu na Odgeri shemasi alianzisha monasteri alimofariki. Anaheshimiwa tangu kale kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Mei.

                                               

Masimo wa Yerusalemu

Masimo wa Yerusalemu alikuwa askofu wa Yerusalemu kuanzia mwaka 333 hivi hadi kifo chake. Wakati wa dhuluma ya kaisari Maximinus Daia alinyofolewa jicho na kuunguzwa mguu, pia alitumwa migodini kufanya kazi ya shokoa. Baadaye alifanywa askofu. Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Mei au 9 Mei.

                                               

Galus wa Clermont-Ferrand

Galus I wa Clermont-Ferrand alikuwa askofu wa 16 wa mji huo kuanzia mwaka 527 hadi kifo chake. Mtoto wa makabaila, alikataa ndoa akawa mmonaki. Kwanza alifanywa padri, halafu askofu, akaongoza kwa ufanisi mkubwa, kama ilivyoandikwa na Gregori wa Tours, aliyekuwa mwanafunzi wake na mwana wa ndugu yake. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 14 Mei.

                                               

Afrodisi wa Afrika Kaskazini

Afrodisi wa Afrika Kaskazini ni kati ya wafiadini wa Kanisa Katoliki waliouawa kikatili sana na Wavandali katika karne ya 5, wakati wa utawala wa mfalme Huneriki aliyekuwa Mwario. Habari za wengi wao zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita. Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu. Sikukuu ya Afrodisi huadhimishwa tarehe 14 Machi.

Zenobi wa Firenze
                                               

Zenobi wa Firenze

Zenobi wa Firenze alikuwa askofu maarufu wa mji huo, aliyejitahidi kuinjilisha eneo lote la kandokando na kupinga Uario. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Mei.

                                               

Niseti wa Vienne

Niseti wa Vienne alikuwa askofu wa 14 au 16 wa mji huo. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Mei.

Mamerto
                                               

Mamerto

Mamerto alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 462 hivi. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Mei.

Kwirino wa Sisak
                                               

Kwirino wa Sisak

Kwirino wa Sisak alikuwa askofu wa Sisak, leo nchini Korasya, aliyeuawa kwa ajili ya imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Galerius kwa kutoswa mtoni amefungwa jiwe shingoni. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 4 Juni

                                               

Leo wa Mantenay

Leo wa Mantenay alikuwa mmonaki aliyepata kuwa abati wa monasteri ya Mantenay-sur-Seine baada ya mwanzilishi wake, Romano kufanywa askofu wa 16 wa Reims. Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Mei.