Back

ⓘ Kuponi
Kuponi
                                     

ⓘ Kuponi

Kuponi, katika mada ya soko na uuzaji, ni tiketi, kijifurushi ama kijikaratasi ambacho kinaweza kukombolewa kwa fedha na kurejeshwa wakati wa ununuzi wa vitu. Kuponi ni njia moja ya kuwapa wateja punguzo la bei kwa bidhaa wanazozinunua.

Kawaida kuponi hutolewa na watengenezaji ili itumike ndani ya uuzaji kama njia moja ya kukuza mauzo. Mara kwa mara husambazwa kupitia bahasha, magazeti, wavuti kama vile mitandao ya kijamii, barua pepe, moja kwa moja kutoka kwa muuzaji, simu kama vile rununu ama simu ya mkononi.

Kuponi hufanya kazi kama vile ubaguzi wa bei, kuwezesha muuzaji kupewa bei iliyo chini kwa wale watumiaji ambao wanaweza kwenda mahala pengine. Kuponi zinaweza kutolewa kwa masoko fulani ambapo kuna ushindani mkubwa. Kwa serikali, kuponi ni kijikaratasi ama kijifurushi ambacho hutumika kwa umuhimu ama ruhusa.

                                     
  • wanafunzi walipanga laini kuchukua vikombe ya milo yao vinywaji kutumia kuponi Milo iliyoongezwa barafu inajulikana kama Milo Peng kwa jina lingine

Users also searched:

...
...
...