Back

ⓘ Kadi ya benki
                                     

ⓘ Kadi ya benki

Kadi ya benki ni kadi ya kufanyia malipo inayoweza kutumika badala ya fedha katika ununuzi. Ni sawa na kadi ya mkopo isipokuwa katika kadi ya debit, pesa huja moja kwa moja kutoka kwenye akaunti ya benki ya mmiliki kadi wakati wa shughuli ya ununuzi. Kadi nyingine zinaweza kubeba dhamana iliyohifadhiwa ambayo hutumika kufanyia malipo ilhali kadi nyingi huwasilisha ujumbe kwa benki iliyotoa kadi ile ili kutoa pesa kutoka akaunti ya mwenye kadi. Mara nyingine nambari ya akaunti yaweza kutumiwa kwenye mitambo ya mtandao pasipo ile kadi plastiki.

Katika nchi nyingi matumizi ya kadi ya debit imetanda kwa kiasi kikubwa na kupiku matumizi ya cheki na kwingineko hadi shughuli za pesa taslimu. Maendeleo ya kadi ya debit tofauti na kadi ya malipo, imekuwa maalum katika nchi, hivyo kusababisha kiwango kikubwa cha shughuli duniani ambazo hazingewiana. Tangu kati ya miaka 2000 nambari kubwa ya watu iliruhusu matumizi ya kadi ya debit kutoka nchi moja kutumika kwa nchi tofauti katika kulipia mtandao na kununulia simu.

Tofauti na kadi ya mkopo na kadi ya malipo, matumizi ya kadi ya debit huwezesha malipo ya papo hapo kutoka akaunti ya mwenye kadi badala ya kulipa kwa siku zitakazofuata. Kadi ya debit pia huruhusu kutoa pesa sawia na kadi ya ATM. Pia mfanyabiashara anaweza kumpa mwenye kadi baki ya fedha iwapo mwenye kadi ametoa pesa kiasi kilichopita bidhaa alizozinunua.

                                     

1. Online debit system / mfumo wa debit ndani ya mtandao

Mfumo huu huhitaji ruhusa ya kieletroniki katika kila shughuli ya malipo ambayo huonyeshwa moja kwa moja katika akaunti ya mwenye kadi. Shughuli hii inawekwa salama na matumizi ya nambari ya siri PIN. Kadi zinginezo pia huhitaji mfumo huo wa nambari ya kisiri katika shughuli yoyote ya kadi hio kama vile kadi ya ATM.

Changamoto ya mfumo huu ni kutokuwepo kwa mashine ya kielectroniki katika kila pahali pa uuzaji.ilhali katika shughuli ya utumizi wa kadi katika nchi nyingi mfumo huu unaonekana bora zaidi kwa sababu ya usalama wake wa uthibitisho ambao huondoa shada ya kuchelewesha shughuli za kifedha.

                                     

2. Offline debit system / mfumo wa debit nje ya mtandao

Mfumo nje ya mtandao una alama ya kadi za mikopo zinazofahamika mfano Visa ama Mastercard ama kadi za debit zinazofahamika mfano Maestro nchini Uingereza na nchi zinginezo pasi na Marekani na hutumika katika shughuli za ununuzi kama kadi ya mkopo na sahihi ya mlipaji. Aina ya kadi ya debit yaweza kuthibitiwa kiasi cha matumizi katika siku au kipimo cha mwisho cha kuangalia baki katika akaunti inayotolewa pesa. Shughuli hizi za nje ya mtandao huchukua siku mbili au tatu kuonyesha baki katika akaunti.

Nchi nyingine, benki na shirika za wafanyabiashara zingine, mkopo wa nje ya mtandao wa kadi ya debit ni shughuli isiyo na malipo ya ziada kwa mnunuzi bali dhamana ya alichokinunua tu. Ilhali shughuli za debit ndani ya mtandao malipo ya ziada hutozwa.

Tofauti nyingine ni kuwa katika shughuli ya debit mtandaoni mnunuzi anaweza kutoa pesa nyingi kuliko alizokusudia kulipia bidhaaiwapo mwanabiashara anakubali tena mwanabiashara hulipa kiwango kidogo katika shughuli mtandaoni kulinganisha na shughuli ya mkopo nje ua mtandao.

                                     

3. Electronic purse card system / mfumo wa kadi ya mfuko wa umeme

Smart-card kadi zenye mfumo wa kielectronikidhamana yake ya kifedha imehifadhiwa kwenye chipu ya kadi na sio akaunti iliyorekodiwa kwa nje. Hivyo basi mashine hukubali kadi pasipo kuunganishwa kwa mtandao hutumika kote Uropa tangu kati miaka ya 1990 sanasana UjerumaniGeldkarte, AustriaQuick Werkarte, NetherlandsChipknip, BelgiumProton, SwitzerlandCASH na UfaransaMoneo ambapo hubebwa na kadi ya debit). nchini Austria na Ujerumani, karibu kila kadi ya benki inahusisha mfuko wa umeme ilhali mfumo huu wa mfuko wa umeme umetolewa juzi nchini Netherlands.

                                     

4. Sifa za kadi ya debit

  • Huwa na ujumbe binafsi wa mmiliki kadi kama vile anwani, jina na nambari ya BINBank Identification number
  • Huweza kuwekwa kwa vitu vya kuchukulia malipo point of sale systems ili kulipia bidhaa alizonunua mmiliki.