Back

ⓘ Mkopo (fedha)
Mkopo (fedha)
                                     

ⓘ Mkopo (fedha)

Mkopo wa kifedha ni pesa ambazo mtu au shirika anapewa na benki, asasi ya fedha ya ushirika, kundi au mashirika mengine yaliyoidhinishwa kufanya biashara ya fedha. Anayepata mkopo huwa na deni analofaa kulipa kulingana na makubaliano rasmi yake na anayemkopesha. Deni hili linaweza kuwa karadha au mkopo unaolipwa pamoja na riba. Riba ndiyo faida ya mashirika kama benki yanayofanya biashara ya ukopeshaji.

                                     

1. Aina za mikopo

Kuna aina nyingi za mikopo kulingana na yanayohitajika kupata ule mkopo, anayelengwa na ule mkopo au lengo la matumizi ya ule mkopo. Mkopo unaweza kuwa fungika - mkopo unaochukuliwa kisha kulipwa kabla ya mtu kuidhinishwa mkopo mwingine - au mkopo endelevu - mkopo unaoweza kuchukuliwa mmoja baada ya mwingine bila hasa kukamilisha kulipa mkopo uliotangulia kama vile mkopo wa kadi ya mkopo credit card.

                                     

1.1. Aina za mikopo Aina za mikopo kulingana na lengo la matumizi

Mashirika tofauti pia hutoa mikopo ya kazi tofautitofauti ikiwemo:

 • Mkopo wa siku mbaya ujulikanao kwa Kiingereza kama payday loans - huu ni mkopo wa hapo kwa papo wakati mtu anahitaji pesa za dharura.
 • Mkopo wa kilimo
 • Mkopo wa nyumba - mikopo inayotolewa ya kununua nyumba hasa katika nchi ambazo biashara ya uuzaji wa nyumba imenawili kama vile Marekani. Nchi nyingine kuna pia mikopo ya kurekebisha na kukarabati nyumba kama vile Singapore.
 • Mkopo wa biashara
 • Mkopo wa matumizi ya binafsi
 • Mkopo wa gari
 • Mkopo wa masomo
 • Mkopo wa kulipa mikopo mingine ujulikanao kwa Kiingereza kama consolidation loan
 • Mkopo wa ardhi na rasilimali nyingine
                                     

1.2. Aina za mikopo Aina za mikopo kulingana na mlengwa

Mashirika yanayofanya biashara ya pesa na idara tofauti za serikali pia yana mikopo inayolenga kundi fulani la watu. Hii ni mikopo kama vile:

 • Mkopo wa wanafunzi
 • Mkopo wa wanajeshi wakongwe
 • Mkopo wa wafanyabiashara
 • Mkopo wa madaktari
 • Mkopo wa wakulima
 • Mkopo wa biashara ndogondogo
 • Mkopo kwa serikali - hii ni mikopo inayolenga serikali na sanasana huhusisha fedha nyingi na riba isiyo ya juu sana.
 • Mkopo wa wafanyakazi wa serikali
 • Mkopo wa walimu
                                     

1.3. Aina za mikopo Aina ya mkopo kulingana na riba inayotozwa

 • Mkopo uliopunguzwa riba hujulikana kwa Kiingereza kama subsidized loans - aina hii ya mkopo hutozwa riba ya chini, kama vile mkopo wa masomo.
                                     

2. Kulipa mikopo

Mkopo ni deni linalofaa kulipwa kulingana na mkataba kati ya anayekopa na anyekopesha. Ikiwa ni mkopo karadha aliyekopa hulipa tu pesa alizokopa ilhali katika mkopo wa riba aliyekopa hulipa mtaji na riba juu yake. Malipo yanaweza kufanyika kidogokidogo kila siku, wiki au mwezi.

Watu wengi hujikuta kwenye shinda za kulipa mikopo na hupoteza mali yao kwa mawakala wa mikopo. Hivyo ni vyema mtu kukopa kwa busara na kutumia mkopo vyema. Kuna mashirika tofauti ambayo huwasaidia watu kutumia na kulipa mikopo yao kwa busara.

                                     

3. Unyanyasaji katika mikopo

Kupeana mikopo kwa minajili isiyo nzuri kama vile kuwapa kwa riba kubwa ambayo wajua vizuri itawafinyilia ni aina mojawapo ya unyanyasaji katika mikopo. Vilevile katika kupeana mikopo, kama hamna mamlaka ambayo inadhibiti na kuona kuwa mkopo wenyewe umetolewa kwa riba fulani, basi huo ni unyanyasaji. Mifano ni payday loans, shylocks na subprime mortage lending.

Kuna vilevile wale ambao huweka riba iwe juu sana kwa sababu anayekopa ana shida anayotaka kutatua papo hapo. Hii huitwa kwa Kiingereza "usury".

Wanaokopa pia huenda wakanyanyasa waliowakopea kwa kutolipa deni lao una kuchelewesha ulipaji.