Back

ⓘ Jamii:Jeshi la Kenya
                                               

Jeshi la Wanamaji la Kenya

Jeshi la Wanamaji la Kenya lilianzishwa tarehe 12 Disemba 1964, mwaka mmoja baada ya Kenya kupata uhuru. Lilitanguliwa na Nevi ya Kifalme ya Afrika ya Mashariki REAN. Baada ya REAN kuvunjwa mwaka 1962, Shirika la Reli na Bandari la Afrika ya Mashariki lilichukua mamlaka ya udhibiti wa shughuli za majini katika maeneo yaliyokuwa makoloni ya Afrika Mashariki hadi nchi huru zikaunda nevi zao. Meja JCJ Kimaro alikuwa Kamanda wa kwanza wa Jeshi la Wanamaji la Kenya. Aliteuliwa na Jomo Kenyatta. Tarehe 4 Septemba 2012 Nevi ya Kenya ilishiriki kuvamia jiji la Kismayo katika juhudi za pamoja za Um ...

                                               

Kings African Rifles

Kings African Rifles ilikuwa jeshi la kikoloni la Uingereza katika Afrika ya Mashariki kati ya mwaka 1902 hadi uhuru wa mataifa ya Kiafrika. Vikosi vyake vilianzishwa Kenya na kupanuka baadaye hadi koloni kwenye maeneo ya Uganda, Tanzania, na Malawi ya leo. Baada ya uhuru vikosi vya KAR katika kila koloni vilikuwa jeshi la nchi huru vikaendelea mwanzoni kwa majina kama Uganda Rifles, Kenya Rifles. Tanganyika Rifles na Malawi Rifles.