Back

ⓘ London School of Economics
London School of Economics
                                     

ⓘ London School of Economics

Chuo kilianzishwa mwaka 1895 mjini London na leo hii ni sehemu ya Chuo Kikuu cha London. Hasa idara ya uchumi ina sifa za kimataifa.

Zaidi ya wakuu wa dola 39 walisoma katika chuo hiki na 8 kati yao wanashika nafasi ya mkuu wa nchi mwaka 2007. Maprofesa pamoja na waliopata digrii chuoni hapa jumla 14 walipokea tuzo ya Nobel ya uchumi, amani au fasihi.

Nafasi za kuendesha utafiti pamoja na nafasi kwa ajili ya wanafunzi huhesabiwa kati ya bora kabisa duniani.

                                     

1. Wanafunzi mashuhuri wa LSE

Kati ya viongozi wa kimataifa waliosoma LSE ni

  • Kwame Nkrumah 1909-1972 - Rais wa kwanza wa Ghana 1960-1966
  • John F. Kennedy rais wa Marekani 1961-1963
  • Mick Jagger mwimbaji wa bendi ya Rolling Stones
  • Jomo Kenyatta 1891-1978 Rais wa kwanza wa Kenya 1964-1978
  • Mwai Kibaki b. 1931 - Rais wa Kenya tangu 2002
  • Romano Prodi waziri Mkuu wa Italia 1996-1998 na tena tangu 2006; 1999-2004 Rais wa Kamati ya Ulaya