Back

ⓘ Nyama choma
Nyama choma
                                     

ⓘ Nyama choma

Nyama choma ni nyama iliyopikwa kwa kuchomwa kwa moto, makaa au jiko la umeme. Pia nyama inaweza kuchomwa na majiko maalum ya kisasa ya gesi ya kuchomea nyama.

Nyama inaweza ama kuchomwa moja kwa moja, ama kwanza kuchemshwa au kupikwa na moshi, mtindo maarufu hasa Marekani, kabla ya kuchomwa.

Harufu yake inavutia watu wengi kuipenda katika nchi na tamaduni mbalimbali duniani. Hivyo imekuwa biashara hasa katika barabara za mijini.

Nyama hii hupendwa pia wakati wa sherehe, matukio muhimu ya kifamilia na marafiki au mwisho wa wiki kwa wale wanaokunywa pombe. Pamoja na kuliwa na vyakula vingine, mara nyingi huandaliwa na kachumbari.

                                     

1. Tofauti za nyama choma duniani

Afrika ya Mashariki

Nyama choma ni maarufu sana Afrika Mashariki, hasa Tanzania na Kenya. Nyama choma katika nchi hizi huitwa mishikaki.

Afrika Kusini

Huko Afrika Kusini nyama huitwa braai kutokana na neno la Kiafrikana "braaivleis."

Uswidi

Nchini Uswidi, kuchoma nyama moja kwa moja kwenye makaa ya moto ndio njia maarufu.

Mexico

Kaskazini mwa Mexico, carne asada ni chakula kikuu. Aina maarufu ni pamoja na arrachera, beefsteak na rib eye, pamoja na chorizo. Kuni na makaa hutumiwa.

Argentina na Uruguay

Huko Argentina na Uruguay, asado nyama iliyochomwa kwenye moto wa wazi na la parrilla nyama ya ngombe iliyochomwa kwenye jiko la asili ni moja ya chakula kikuu.

                                     

1.1. Tofauti za nyama choma duniani Afrika Kusini

Huko Afrika Kusini nyama huitwa braai kutokana na neno la Kiafrikana "braaivleis."

                                     

1.2. Tofauti za nyama choma duniani Namibia

Nchini Namibia, nyama choma ambayo huitwa kapana huchomwa kwa moto wa kuni. Nyama hii hukatwa vipande vidogo na kuchomwa sio zaidi ya dakika 10. Ni nyama maarufu sana kwenye masoko na sehemu za starehe.

                                     

1.3. Tofauti za nyama choma duniani Uswidi

Nchini Uswidi, kuchoma nyama moja kwa moja kwenye makaa ya moto ndio njia maarufu.

                                     

1.4. Tofauti za nyama choma duniani Mexico

Kaskazini mwa Mexico, carne asada ni chakula kikuu. Aina maarufu ni pamoja na arrachera, beefsteak na rib eye, pamoja na chorizo. Kuni na makaa hutumiwa.

                                     

1.5. Tofauti za nyama choma duniani Argentina na Uruguay

Huko Argentina na Uruguay, asado nyama iliyochomwa kwenye moto wa wazi na la parrilla nyama ya ngombe iliyochomwa kwenye jiko la asili ni moja ya chakula kikuu.

                                     

1.6. Tofauti za nyama choma duniani Japani

Kwenye miji ya nchini Japani, mikokoteni ya yakitori, migahawa au madukani, nyama chomwa huuzwa. Nyama iliyolainishwa kwa marinadi huchomwa kwenye jiko la mkaa kwa kutumia vijiti. Huko Malaysia, Singapore, Indonesia, na Thailand, nyama choma iitwayo satay, ambayo ni nyama iliyolainishwa na kuchomwa kwa makaa kisha huliwa na karangawhich is marinated meat on a bamboo skewer grilled over a charcoal fire and served with peanut sate sauce.

                                     

2. Athari za kiafya

Utafiti unaonyesha kuwa kuchoma nyama kwa joto la juu kunaweza kusababisha magonjwa mbalimbali. Lakini kulainisha nyama kwa kutumia marinadi kunaweza kupunguza hatari ya magonjwa hayo.

Nyama chooma huaminika kuwa njia mbadala bora ya kupika kuliko kutumia mafuta, ingawa uchomaji unaweza kufanya nyama kuwa kavu.