Back

ⓘ Mkataba wa Kimberley
Mkataba wa Kimberley
                                     

ⓘ Mkataba wa Kimberley

Mkataba wa Kimberley ni mchakato ulioanzishwa mnamo mwaka wa 2000 ili kuzuia "almasi za damu" kuingia katika soko kuu la biashara ya almasi.

Mchakato huu ulitolewa na Suluhisho la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kifungu cha 55/56 kwa kufuatia mapendekezo yaliyotolewa katika Ripoti ya Fowler. Mchakato ulilenga kuhakikisha ya kwamba "manunuzi yote ya almasi hayafadhili machafuko wala vikundi vya waasi na washirika wao wanaotaka kuitoa serikali halali madarakani"

Ufanisi wa mchakato ulizua maswali kadhaa kutoka kwa asasi mbalimbali ikiwa moja wapo ni Global Witness, ambao walijitoa katika mpango huu mnamo tarehe 5 Desemba 2011, wakidai ya kwamba imeshindwa kutumiza malengo yake na haitoi masoko ya uhakika ambayo si ya almasi za mgogoro.

                                     

1. Historia

Umoja wa Mataifa ilipitisha mapendekezo yake dhidi ya UNITA mnamo mwaka 1998 kupitia Baraza la Usalama na Usulushi la Umoja wa Mataifa kifungu nambari 11773, pamoja na hayo, wachunguzi waliokuwa wanaongozwa na Robert Fowler waliwasilisha mrejesho wa Ripoti ya Fowler kwa UM mnamo mwezi Machi 2000, ambayo ilieleza namna ambavyo ushafirishwaji ulivyokuwa unawezesha kufadhili jitahada za kuchochea vita kupitia fedha wanazopata katika mauzo ya almasi kwenye soko la kimataifa. Umoja wa Mataifa ulitaka kukata mzizi wa fitna katika biashara hii, lakini hawakuwa na uwezo wa kuyatekeleza haya; hivyo basi ripoti ya Fowler ilitaja majina ya nchi, makampuni, serikali na watu binafsi waliokuwa wanajihusisha na almasi za mgogoro. Jambo hili lilipelekea kufanyika mkutano wa nchi za Afrika ya Kusini zinazojishughulisha na uchimbaji wa madini ya almasi na mkutano ulifanyika mnamo mwezi Mei 2000 huko Kimberley, Northern Cape. Hitimisho la mkutano lilifuatiwa mnamo mwezi wa Septemba huko mjini Pretoria, ambapo KPCS ndipo inapotokea.

Mwezi wa Disemba 2000, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio lake kwa kutumia vifungu vya "Resolution A/RES/55/56, wakiunga mkono suala la kuundwa kwa skimu ya cheti maalumu cha kimataifa cha kusimamia almasi ghafi zote, hili liliafuatiwa na kuungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika usuluhishi wake kifungu nambari 1459 kwa kupitisha mnamo mwezi wa Januari 2003. Kila mwaka tangu kupitishwa kwa azimio, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa hupitisha upya mkakati huu, mara ya mwisho ilikuwa mwaka Disemba 2009.

Ili nchi iwe mwanachama, lazima ihakikisha ya kwamba almasi inayotoka nchini mwake haifadhili vikosi vya uasi au shirika lolote lile ambalo linataka kuitoa madarakani serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, na kwamba kila almasi itakayosafirishwa lazima iambatane na nyaraka za Mchakato wa Kimberley na kwamba hakuna almasi itakayosafirishwa nje, au kuingizwa, katika nchi ambayo si mwanachama wa skimu hii. Hatua hizi tatu zimewekwa mahususi kuhakikisha ya kwamba nchi zitakazo husika na shughuli za almasi zisizo na mgogoro. Kwa kuweka mipaka maalumu ya mapato ya almasi kwa vyanzo vilivyothibishwa na serikali pekee, Mchakato wa Kimberley haugemei na sera ya dhidi ya serikali nyengine.

                                     

2.1. Masharti Mfumo wa hati za uthibitisho

Baraza la Almasi la Dunia limeazisha Mfumo wa Hati za Uthibitisho kwa ajili ya almasi ambazo zimeidhinishwa na wanachama wote wa KPCS. Chini ya mfumo huu, wauzaji na wanunuzi wa almasi ghafi na zilizosafishwa wanalazimika kuthibitisha taarifa zifuatazo katika ankara zote za malipo yao:

Almasi hizi zilizolipiwa zimenunuliwa kutoka katika vyanzo halali na hazihusiki na kufadhili migogoro na zinakubaliana na azimio la usuluhishi wa Umoja wa Mataifa. Muuzaji anathibitisha ya kwamba almasi hizi hazina mgogoro, kwa mujibu wa ufahamu binafsi na maanadishi yaliyoandikwa anathibitisha almasi iliyotolewa haina shaka ndani yake.”

Huhesabiwa kama ukiukwaji wa utaratibu wa KPCS kutoa tangazo la hati za uthibitisho katika ankara ya mauzo isipokuwa kama itaweza-kuthibitika na hati za manunuzi zilizopokelewa. Kila kampuni inayofanya biashara ya kuuza almasi zinalazimika kutunza kumbukumbu za hati za uthibitisho walizopokea na hati za uthibitisho za ankara watakazoa kwa ajili ya kuuza au kununua almasi. Mtiririko wa hati za uthibitsho zinatoka na kuingia lazima zikaguliwe na zioane kazi ambayo inatakiwa ifanywe kila mwaka na wakaguzi wa kampuni.

Isitoshe, makampuni na mashirika ya almasi na wanachama wake wanatakiwa wafuate utaratibu unaofuata katika kujiwekea kanuni za ndani ya shirika:

 • kununua au kuuza kwa kutokujua na kuwauzia wengine almasi zenye mgogoro;
 • kuhakikisha ya kwamba waajiriwa wa kampuni ambao wananunua au kuuza almasi wanatakiwa wawe na taarifa za kutosha kuhusu azimio la kibiashara na serikali katika kuzuia ununuzi na uuzwaji wa almasi zenye mgogoro.
 • kufanya biashara na kampuni ambazo zinataja hati za uthibitisho kwenye ankara zao;
 • kutonunua almasi kutoka katika ukanda ambao serikali imeumeuna kuzalisha almasi zenye mgogoroto na hafuati taratibu za Kimberley;
 • kutonunua almasi kutoka kwenye vyanzo vyovyote ambavyo, baada ya mchakato wa kisheria kupita, lakini wakakutanika na ukiukwaji wa utaratibu uliowekwa na serikali ambao wa kuzuia kufanya biashara ya almasi zenye mgogoro;
 • kutonunua almasi kutoka katika vyanzo vyenye mashaka au wauzaji wasiotambulika, au inatoka katika nchi ambazo hazijatimiza mchakato wa Kimberley;

Kushindwa kutimiza haya na mwanachama akigundulika kufanya tofauti atafukuza kutoka katika jumuia.

                                     

3. Wanachama wa sasa

Hadi tarehe 1 Julai 2013, kulikuwa na washiriki 54 wa KPCS ambao wanawakilisha nchi 81, huku Umoja wa Ulaya ukihesabiwa kama mwanachama mmoja. Washiriki wamejumlishwa wote wanaozalisha almasi ghafi na kamili, nchi zinazosafirisha au kuingiza. Hivi karibuni, Cameroon ilikubali kuwa mwanachama mnamo Agosti 2012 pamoja na Kazakhstan, Panama, na Cambodia waliingia mwezi wa Novemba 2012.

Orodha ifuatayo ni nchi wanachama walioshiriki na miaka yao ya kuingia, kuingia tena kama utaratibu unavyotaka mabano mwaka alioingia.

Waombaji

Nchi zifuatazo ni zile ambazo zimeonesha shauku ya kutaka kujiunga na KPCS, lakini bado hawajatimiza malengo:

 • Mozambique
 • Zambia
 • Burkina Faso
 • Mauritania
 • Mali
 • Kenya
 • Chile
                                     

4. Viungo vya nje

 • World Centers of Compassion for Children International
 • A transcript of the Clean Diamond Act Archived Oktoba 23, 2016 at the Wayback Machine.
 • Civil Society Groups warn effectiveness of Kimberley Process compromised
 • kimberleyprocess.com
 • AFRICAN DIAMOND COUNCIL - Africas official diamond governing body
 • kimberly certified diamonds
 • Facts about non-conflict diamonds from the World Diamond Council