ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 63
                                               

Makumbusho ya Nayuma

Makumbusho ya Nayuma ni makumbusho yanayopatikana katika jiji la Mongu, mkoa wa Magharibi, nchini Zambia. Makumbusho hayo ni kwa ajili ya kukuza sanaa na kazi za kisanii ya Balotseland hasa.

                                               

Makumbusho ya Reli (Zambia)

Makumbusho ya Reli ni makumbusho yaliyoko Livingstone, Zambia. Ni jumba la kumbukumbu lililotoleWa kuhifadhi urithi wa reli ya Zambia, na vilevile kufanya maonyesho juu ya historia ya mbio za Kiyahudi huko Zambia.

                                               

Marjarini

Marjarini ni mafuta ya kuliwa yaliyobuniwa kama mbadala wa siagi. Iko katika hali laini kiasi, ili iweze kupakuliwa kwa jotoridi la wastani. Hutengenezwa kwa kutumia uto au pia kwa kutumia mafuta ya nyama. Inaweza pia kuwa na unga wa maziwa, chum ...

                                               

Matamasha Makuu ya Afrika Mashariki

Mombasa Carnival ni tamasha lifanyikalo katika mji wa Mombasa, nchini Kenya, ambalo huonyesha historia, utamaduni, na muziki vya Mombasa na nchi ya Kenya kwa jumla. Mombasa ni mji wa pwani, wa pili kwa ukubwa ndani ya Kenya ina historia kubwa san ...

                                               

Mavazi

Mavazi ni nguo ambazo huvaliwa na watu ili kufunika mwili au sehemu zake. Mavazi huwa na makusudi mbalimbali: huwasilisha ujumbe kwa watu wengine kwa kuonyesha mtu fulani ni sehemu ya kundi au tabaka nguo ghali za tajiri au anapendelea jambo nemb ...

                                               

Mbege

Mbege ni pombe ya asili ya Wachagga, wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro. Mbege hutengenezwa na ndizi mbivu, ulezi, na maji. Mara nyingi mbege hutengenezwa na wanawake na hutumika katika sherehe na matukio mbalimbali kama vile harusi, misiba, ubarikio, ...

                                               

Wambugu

Wambugu ni kabila linalopatikana katika wilaya ya Lushoto ambako wanaishi katika makundi katikati ya jamii ya Wasambaa. Maeneo wanakopatikana kwa wingi ni Kwemakame, Mazumbai, Kinko, Rangwi, Msare, Mavumo, Kitanga na Magamba na sehemu nyingine, A ...

                                               

Mfalme Arthur

Mfalme Arthur ni mhusika mashuhuri katika masimulizi ya mitholojia ya Britania. Anakumbukwa kama mfalme aliyeishi katika kasri yake ya Camelot akiwa na upanga wake unaojulikana kama Excalibur, aliopewa na Bibi wa Ziwa. Katika kumbukumbu hiyo Arth ...

                                               

Mkate

Mkate ni chakula kinachotengenezwa kwa kuoka kinyunga cha unga na maji. Mara nyingi viungo fulanifulani huongezwa kwa kubadilisha ladha. Kuna pia mikate inayotiwa kiasi kidogo cha mafuta.

                                               

Mnazi (kinywaji)

Mnazi ni pombe inayotengenezwa na utomvu wa nazi changa iliyogemwa ikiwa mtini. Utomvu huu ukikusanywa ndio unaotoa pombe ya mnazi. Pombe hii ya mnazi ni maarufu sana maeneo ya mwambao wa pwani Tanzania ambapo minazi huota kwa wingi hasa Tanga. P ...

                                               

Mona Lisa

Mona Lisa ni mchoro maarufu wa mwanzoni mwa karne ya 16, kazi ya na mwanasayansi na mchoraji Leonardo da Vinci. Inaaminika kuwa ni mmoja kati ya michoro mashuhuri zaidi duniani kote. Kwa sasa mchoro huu unapatikana katika jumba la maonyesho makum ...

                                               

Msesewe

Wapikaji pombe wanabandua magamba ya msesewe, wanaanika kwenye jua, wanayapigapiga mpaka yawe vipande vidogovidogo, ambavyo hupelekwa mashineni kwa kusaga na kuwa katika hali ya unga.

                                               

Mtayarishaji wa filamu

Mtayarishaji wa filamu ni mtu anayeanzisha mandhari ya utengenezaji wa filamu. Mtayarishaji hutazama na kudhibiti vitu kama vile upatikanaji wa fedha ili kutengeneza filamu, kuajiri watu, na kupanga maandalizi ya kupeleka filamu kwa wasabambazaji ...

                                               

Nyanya chungu

Nyanya chungu ni tunda la mngogwe, jamii ya mbiringani, ambalo linatumika kama mboga. Ina wingi wa vitamini A, B, C, K na madini, hivyo inasaidia sana afya. Ina ladha chunguchungu na huliwa kwa ugali, lakini ngogwe Habeshi inaweza kuliwa mbichi p ...

                                               

Nyumba ya Arewa

Nyumba ya Arewa ni kituo cha utafiti na historia kilichopo chini ya chuo kikuu "Ahmadu Bello University", nchini Nigeria. Makumbusho hayo yapo katika mji wa Kaduna

                                               

Nyumba ya Chilenje 394

Nyumba ya Chilenje 394 ni makumbusho yanayopatikana katika eneo la Chilenje, Lusaka nchini Zambia. Nyumba hiyo ilikuwa makazi ya Kenneth Kaunda aliyeishi hapo kuanzia Januari 1960 hadi Disemba 1962, na baadaye kuja kuwa rais wa kwanza wa nchi ya ...

                                               

Nyumba ya Utopia

Nyumba ya Utopia ni nyumba ya makumbusho ya kihistoria yanayopatikana katika jiji la Zimbabwe yakiwa ni jumba la kwanza la kisasa kujengwa mwaka 1897. Hapo awali ilikuwa nyumba ya Rhys Fairbridge, mmoja wa walowezi Wazungu wa mapema katika eneo h ...

                                               

Ofisi

Ofisi kwa ujumla ni chumba au eneo lingine ambalo kazi ya utawala hufanywa, lakini pia inaweza kuonyesha nafasi katika shirika na kazi maalum zinazohusiana nayo kutimiza wajibu wa mtu. Katika hali ya sasa ofisi kawaida inahusu sehemu ambako huaji ...

                                               

Pambo

Pambo ni kitu au kifaa kinachotumika kuongezea urembo au uzuri wa mtu, nyumba, au kitu kingine chochote. Tangu zamani za kale binadamu ameonyesha kipaji chake cha usanii kwa kupamba vitu mbalimbali, hasa vile vinavyomhusu zaidi, kama vile mavazi ...

                                               

Pasta

Pasta ni neno lenye asili ya Kiitalia kinachojumlisha chakula cha tambi kilichotengenzewa kwa kutumia unga wa nafaka na maji. Aina ya pasta inayofahamika zaidi ni spaghetti. Lakini kuna aina nyingi za pasta. Chanzo cha pasta hufanana kiasi na uga ...

                                               

Pilau

Pilau, ni mlo ambao nafaka, kama vile mchele au ngano uliopasuliwa, hubadilishwa rangi kuwa hudhurungi katika mafuta, na kisha hupikwa katika supu ambayo ina ladha. Kutegemeana na vyakula vya eneo husika, pilau inaweza kujumuisha aina mbalimbali ...

                                               

Pizza

Pizza ni chakula chenye asili ya Italia kilichosambaa kote duniani. Ni kipande cha mkate bapa kinachofunikwa kwa mchuzi mnene wa nyanya na vipande vya jibini. Mara nyingi vipande vyembamba vya mboga mbalimbali, nyama au samaki vinaongezwa pamoja ...

                                               

Sana Maulit Muli

Sana Maulit Muli ni jina la kutaja tamthiliya ya Kifilipino iliyokuwa ikirushwa hewani-kutayarishwa na kituo cha televisheni cha ABS-CBN. Inasadikika kuwa kilikuwa moja kati vipindi vya televisheni vilivyokuwa vikitazamwa sana huko nchini Ufilipi ...

                                               

Sanaa ya mapigano

Sanaa za mapigano zilitokea katika jamii nyingi duniani pale ambapo watu walipaswa kupigana kati yao. Hapo wapiganaji wenye uwezo walianza kuwafundisha wengine namna ya kushika fimbo, upanga, upinde na silaha za kila aina, namna ya kulenga, namna ...

                                               

Sanamu

Sanamu ni kazi ya sanaa ambayo inatofautiana na picha au mchoro kwa sababu inaonyesha mtu au kitu si kwa urefu na upana, bali pia kwa unene. Inaweza kutengenezwa kwa kuchonga au kwa njia nyingine k.mf. kumimina kiowevu katika muundo uliokusudiwa.

                                               

Shikamoo

Shikamoo ni neno linalotumiwa kumsabahi mtu. Ni salamu inayotumiwa na wadogo kwa wakubwa wao, hasa wale wanaowazidi umri. Jibu lake ni "Marahaba". Maana ya neno huelezwa kuwa kifupi cha "nashika mguu wako" kama tamko la heshima mbele ya mkubwa. J ...

                                               

Siagi ya karanga

Siagi ya karanga ni chakula chenye umbo la malai ambayo inatengenezwa kwa kutumia karanga zilizokaangwa. Karanga zinasafishwa baada ya kukaangwa halafu zinasagwa. Wakati wa kusaga mafuta yaliyopo ndani yake yanatoka; kama hamna ya kutosha, mafuta ...

                                               

Siku ya Kitaifa ya ushairi

Siku ya Kitaifa ya Ushairi ni kampeni inayofanyika nchini Uingereza kwa ajili ya kuutangaza ushairi, ikijumuisha maonyesho ya wazi. Siku ya kitaifa ya ushairi ilianzishwa mwaka 1994 na William Sieghart. na hufanyika kila mwaka katika nchi za UK n ...

                                               

Siku ya Ushairi Duniani

Siku ya Ushairi Duniani husherehekewa kila mwaka tarehe 21 Machi. Ilipitishwa rasmi na shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO Shirika la Elimu, sayansi na utamaduni mnamo mwaka 1999 ili "kuunga mkono lugha tofauti kupitia ushairi na kuongeza fursa ...

                                               

Steph-Nora Okere

Steph-Nora Okere ni mwigizaji na mwandishi wa Nigeria ambaye alipewa Tuzo Maalum ya Utambuzi kwenye Tuzo za City People Entertainment Awards mnamo mwaka 2016. Mnamo mwaka 2015 Okere alikua Makamu wa Rais wa Chama cha Waandishi wa Hati wa Nigeria.

                                               

Stephanie Okereke Linus

Stephanie Linus. Ni mwigizaji filamu wa Kike wa Nigeria,pia ni mwongozaji wa filamu na mwanamitindo. Alipata tuzo na teuzi mbalimbali kutokana na kazi yake ya uigizaji, ikiwemo tuzo ya Reel mwaka 2013 kama mwigizaji bora wa kike, tuzo ya Afro Hol ...

                                               

Suruali

Suruali ni vazi linaloshonwa na linalovaliwa kutoka kiunoni hadi miguuni chini na lenye nafasi mbili zinazotenganishwa kupenyezea miguu. Kwa asili ni nguo ya wanaume, lakini inavaliwa na wanawake pia mradi yamefanyika mabadiliko kadhaa katika ush ...

                                               

Sweta

Sweta ni vazi au nguo inayovaliwa hasa kipindi cha baridi kwa ajili ya kutunza joto la mwili katika kifua na mikono. Huvaliwa katika sehemu zenye baridi kidogo, kwa sababu katika sehemu zenye baridi kali watu hupendelea kuvaa makoti kwa kuwa yana ...

                                               

Tacos ya Ufaransa

Tacos ya Kifaransa ni chakula chenye tortilla ya ngano inayoviringishwa imejaa vibanzi vya viazi, jibini na nyama., vibanzi na mchuzi. Ingawa chakula hicho kinaitwa kwa jina la Kihispania "tacos", ni tofauti na tacos za Meksiko ilhali kinafanana ...

                                               

Taj Mahal

Taj Mahal ni jengo zuri la kaburi lenye umbo la msikiti mjini Agra. Mara nyingi huhesabiwa kati ya majengo mazuri duniani. Taj Mahal ilijengwa 1631 - 1648 kwa amri ya Shah Jahan aliyekuwa mtawala wa nasaba ya Moghul aliyetaka kumkumbuka mke wake ...

                                               

Tambi

Tambi ni chakula kinachotengenezwa kutoka kwa kinyunga cha unga na maji kuwa kama milia membamba inayopikwa katika maji au supu. Ni chakula muhimu katika nchi nyingi hasa Italia, China, Japani na Korea. Siku hizi zimeenea kote duniani. Aina zinaz ...

                                               

Terakota

Terakota ni sanaa na vifaa vya ufinyanzi vinavyotengenezwa kwa kutumia udongo mwekundu unaochomwa, mara nyingi bila ganda la kioo usoni mwake. Jina limetokana na neno la Kiitalia terracotta "udongo uliochomwa". Kimsingi hakuna tofauti kubwa kati ...

                                               

Togwa

Togwa ni kinywaji baridi kinachotengenezwa kwa nafaka au maji ya matunda. Namna ya kutengeneza ni sawa na pombe ya kawaida ila tu haikubadilika bado kuwa na alikoholi. Togwa ndiyo itakuwa pombe ikikaa. Kwa mfano, togwa ya ulanzi ni utomvu kutoka ...

                                               

Tortilla

Tortilla ni aina ya mkate bapa wa Meksiko unaofanana na chapati. Kwa kawaida hutengenezwa kwa unga wa mahindi lakini siku hizi kuna pia tortilla za ngano. Wamexiko huandaa mahindi kwa kuyapika katika maji walimotia kiasi cha chokaa na kuikoboa ba ...

                                               

Troli wa mtandaoni

Kwenye misemo ya mtandaoni, troli ni mtu anayeanzisha ugomvi au anayekasirisha watu kwa kutoa maoni yanayovuruga majadiliano na kugombanisha watu. kwenye majukwaa ya mtandaoni, vyumba vya majadiliano, au blogu kwa nia ya kuchokoza wasomaji. Miaka ...

                                               

Ubuntu

Ubuntu ni falsafa ya Kiafrika inayosisitiza mahusiano na ushirikiano wa jamii kama msingi wa maisha bora na amani katika jamii. Falsafa hii inaonesha nafasi ya mtu katika jamii iliyomzunguka. Ushirikiano ni njia bora ya kuishi kama jamii kuliko u ...

                                               

Uchoraji

Kuhusu nyota angalia hapa Mchoraji Uchoraji ni sanaa ya kuweka alama au picha kwa kutumia vifaa mbalimbali vya kuchorea, kama vile kalamu ya wino au ya risasi, burashi, penseli za rangi ya nta, crayoni, makaa, choko, pastels, aina mbalimbali za e ...

                                               

Ugali

Ugali ni chakula kinacholiwa na jamii za kiafrika. Chakula hiki chenye virutubisho vya wanga hutokana na unga wa nafaka au muhogo. Ugali hutayarishwa kwa njia ifuatayo: kwanza unachemsha maji kwenye sufuria baada ya kuchemka unachanganya unga kid ...

                                               

Uigizaji wa sauti

Uigizaji wa sauti ni sanaa ya kutoa au kuigizia sauti ya uhusika wa katuni redio na maigizo ya sauti na vichekesho, kufanyia sauti juu yake kwenye redio na televisheni, michezo ya redio, kuigizia sauti za washiriki wa kwenye filamu za lugha za ki ...

                                               

Uji

Uji ni kinywaji kinachopikwa kwa kuchemsha unga na maji ukawa laini. Mara nyingi hupendwa asubuhi na kwa ajili ya watoto na wagonjwa. Unga unaotumika unaweza kuwa wa mahindi, lakini pia mtama, ulezi, uwele n.k.

                                               

Ukuta

Kwa makala juu ya taasisi ya UKUTA, nenda UKUTA. Ukuta ni muundo wima unaopakanisha nafasi kuwa tofauti, kama maeneo ya ndani na nje au vyumba ndani ya jengo.

                                               

Ulaji mboga

Ulaji mboga ni namna ya maisha inayoepuka vyakula vinavyotokana na wanyama waliouawa, kama vile nyama na samaki. Watu wanaokataa kula nyama huitwa wala mboga vegetarians, wakitumia mboga, matunda, majani, nafaka, jozi na mbegu mbalimbali. Mara ny ...

                                               

Usanifu wa ndani

Usanifu wa ndani ni sanaa na sayansi ya kuboresha muonekano wa ndani ya nyumba au jengo lolote, wakati mwingine ikiwa ni pamoja na nje, kufikia mazingira bora na yenye kupendeza kwa mtumiaji. Msanifu wa ndani ni mtu ambaye anapanga, anatafiti, an ...

                                               

Vampiri

Vampiri ni madubwana katika hadithi na hekaya. Hadithi za kwanza za vampiri zilihadithiwa huko Ulaya Mashariki, lakini watu wengi wanadhani vampiri waliundwa na Bram Stoker katika riwaya maarufu, Dracula. Watu wachache wanaamini kuwa vampiri wana ...

                                               

Vibanzi

Vibanzi ni aina ya chakula kinachotayarishwa kwa viazi au viazi vikuu. Katika uandaaji wa chakula hiki viazi hukatwa kwa vipande vyembamba vilivyooshwa na kuwekwa kwenye mafuta ili viweze kuiva na kuliwa. Kwa kawaida hukaangwa mara mbili, mara ya ...