ⓘ Free online encyclopedia. Did you know? page 60
                                               

Mianga ya aurora

Mianga ya aurora ni mianga ya rangi mbalimbali inayotokea katika matabaka ya juu ya angahewa. Hutazamwa kwa kawaida katika sehemu za Dunia zilizo karibu na ncha ya kaskazini au ya kusini. Kwa Kilatini mianga hiyo ikitokea karibu na ncha ya kaskaz ...

                                               

Milima kunjamano

Milima kunjamano ni aina ya milima ambayo hutokea wakati mabamba ya gandunia yanagongana. Shinikizo linasababisha kukunjwa kwa ganda la dunia na hili linafanya sehemu ya uso wa ardhi kuinuliwa juu. Tokeo lake ni safu ya milima au pia mfululizo wa ...

                                               

Milimita ya ujazo

Milimita ya ujazo ni kipimo cha mjao kinacholingana na mchemraba wenye urefu, upana na kimo cha milimita 1. Alama yake ni mm³. Hii ni sawa na sehemu ya bilioni ya mita ya ujazo na sawa na mikrolita μl. 1 mm³ ni sawa na 0.000 001 dm³ 0.001 cm³ 0.0 ...

                                               

Minciu Sodas

Minciu Sodas ni maabara ya kiteknolojia inayoendeshwa kwa njia ya intaneti yenye lengo la kuunganisha watu, vikundi na hata makampuni kwa kulenga mitazamo yao na michango yao katika jamii. Maabara hii huwahusishwa vijana, wamama, walemavu, wakuli ...

                                               

Mipindopindo (mto)

Mipindopindo ni umbo la mto wenye vizingo vingi. Mipindipindo hutokea pale ambako mto unapita katika tambarare yenye ardhi laini bila mteremko mkubwa. Mipindopindo hubadilika baada ya muda kwa namna inayofanana na mwendo wa nyoka. Mipindopindo hu ...

                                               

Mishipa ya damu

Mishipa ya damu ni mabomba ndani ya mwili ambamo damu inasafirishwa pande zote za mwili. Pamoja na moyo inaunda mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Vena ni mishipa inayopeleka damu kuingia moyoni kutoka mwilini. Ateri ni mishipa inayopeleka damu k ...

                                               

Mita ya ujazo

Mita ya ujazo ni kipimo cha mjao chenye urefu, upana na kimo cha mita moja. Ni kiwango katika vipimo vya SI. Jina lingine ni "kilolita". Mita moja ya ujazo inalingana na lita 1.000 au sentimita za ujazo 1.000.000. 1 m³ ya maji safi katika hali sa ...

                                               

Mjao

Mjao unaeleza ukubwa wa gimba la hisabati kwa kupima nafasi ya yaliyomo yake. Hupimwa katika vizio vya ujazo kama mita ujazo m³ au sentimita ujazo cm³. Kila gimba lenye urefu, upana na kimo huwa na mjao. Alama yake ni V. Hali halisi ni kwamba nje ...

                                               

Mngaro wa Jua

Mngaro wa Jua ni jumla ya mngaro au mnururisho wa sumakuumeme unaotoka kwenye Jua na kuelekea nje yake katika anga-nje pande zote. Hii ni pamoja na wimbiredio, mikrowevu, mawimbi ya joto, eksirei, na nuru inayoonekana kwetu. Mngaro huo huwa na ki ...

                                               

Mpito wa sayari

Mpito wa sayari unamaanisha hali ya sayari kupita kati ya Jua na Dunia na hivyo kufunika sehemu ya Jua. Tofauti haionekani kwa macho lakini inaweza kutazamwa kwa kutumia darubini. Kuna sayari mbili zinazoweza kupita mbele ya Jua kwa macho ya mtaz ...

                                               

Mshtarii

Mshtarii ni sayari ya tano toka kwenye jua katika Mfumo wa jua na sayari zake. Mshtarii ni sayari kubwa kabisa ya jua letu. Masi yake inazidi mara mbili na nusu masi ya sayari zingine zote pamoja.

                                               

Msitu wa mvua

Msitu wa mvua ni msitu unaopokea mvua nyingi yaani usimbishaji wa zaidi ya milimita 2.000 kwa mwaka. Kwa hiyo msitu unastawi vizuri kuna aina nyingi za mimea na wanyama kushinda misitu mingine. Kuna namna mbili za misitu hii kutokana na halijoto: ...

                                               

Msuguano

Msuguano ni hali ya kitu kutokukubaliana na mwendo wa vitu vigumu, vitu vya kimiminika na vitu vinavyosuguana vyenyewe. Kuna aina mbalimbali za misuguano: Msuguano mkavu ni msuguano wa vitu viwili vyenye asili ya ugumu pamoja. Msuguano mkavu umeg ...

                                               

Mtapo

Mtapo ni mwamba asilia au mashapo yenye madini ya thamani ndani yake, hasa yenye metali ndani yake. Mtapo hupatikana katika ardhi au chini ya ardhi au ndani ya mlima ukitolewa kwa kuuchimba, mara nyingi katika migodi. Baadaye madini yanayotafutwa ...

                                               

Mvua

Mvua ni matone ya maji yanayoanguka chini kutoka mawingu angani. Mvua ni aina ya usimbishaji. Kama matone yafikia kipenyo cha zaidi ya milimita 0.5 huitwa mvua. Kama matone ni madogo zaidi kunaitwa manyonyota. Mgongoni mwa ardhi mvua imetapaka ki ...

                                               

Mvua ya mawe

Mvua ya mawe ni aina ya mvua ambayo matone ya maji yamefika kwenye uso wa ardhi kwa umbo la vipande vya barafu. Inatokea wakati matone ya maji ya mvua yanapita kwenye hewa baridi na kuganda hadi kuwa barafu. Hali halisi mvua inayonyesha si mawe b ...

                                               

Mwaka mpya

Mwaka mpya ni siku ya kwanza ya mwaka na mara nyingi ni sherehe na nafasi ya watu kutakiana heri na baraka za mwaka mpya. Katika tamaduni mbalimbali nafasi hii ni sikukuu moja au zaidi pasipo na kazi za kawaida.

                                               

Mwamba (jiolojia)

Mwamba katika jiolojia ni namna ya kutaja mawe au zaidi mchanganyiko au mkusanyiko wa mabao ya aina moja au zaidi ya madini ulio imara katika hali asilia. Jiwe ni kipande cha mwamba. Takriban madini 30 hufanya sehemu kubwa ya miamba ya dunia, ni ...

                                               

Mwamba mashapo

Miamba mashapo hutokea pale ambapo mashapo hukaa kwa muda mrefu yakifunikwa na mashapo mengine na kuathiriwa na uzito wa matabaka ya juu yanayosababisha shinikizo kubwa. Miamba ya aina hiyo hufanya sehemu kubwa ya uso wa ardhi, ingawa Dunia kwa j ...

                                               

Mwamba metamofia

Mwamba metamofia ni aina ya mwamba ambao umebadilishwa na joto kali na shinikizo kubwa. Jina latokana na ing. metamorphic iliyochukuliwa kutoka Kigiriki morph na meta. Mwamba wa asili unaathiriwa na joto zaidi ya °C 150 hadi 200 na shinikizo la b ...

                                               

Mwamba wa mgando

Mwamba wa mgando ni moja ya aina tatu kuu za miamba, pamoja na mwamba mashapo na mwamba metamofia. Miamba ya mgando huundwa kutokana kwa kupoa kwa magma au lava, yaani mwamba moto katika hali ya kiowevu jinsi inavyopatikana katika koti la Dunia. ...

                                               

Mwambatope

Mwambatope ni aina ya mwamba mashapo yenye chembe ndogo sana; asili yake ni mashapo ya matope. Matope yanayofanya mwambatope ni ya udongo wa mfinyanzi clay pamoja na chembe ndogo za kwatzi na kalsiti. Mara nyingi mwambatope yanatokea kwa matabaka ...

                                               

Mwangaza halisi

Mwangaza halisi ni kipimo cha ukali wa nuru ya nyota au magimba mengine ya anga jinsi itakavyoonekana kwa mtazamaji aliye kwa umbali sanifu wa miakanuru 32.6 au parsek 10. Mwangaza halisi ni tofauti na mwangaza unaoonekana jinsi tunavyoona nyota ...

                                               

Mwezi

Mwezi ni gimba la angani linalozunguka sayari fulani. Kuna miezi mingi katika anga-nje. Vipindi vya kuonekana kwa mwezi wa Dunia vilisababisha matumizi ya "mwezi" kama majira ya wakati. Mabadiliko ya kuonekana kwake yalisababisha katika Kiswahili ...

                                               

Myeyungano wa kinyuklia

Myeyungano wa kinyuklia ni mchakato ambamo viini 2 au zaidi vya atomu vyepesi zaidi vinaungana kuwa kiini kimoja kizito. Masi ya kiini cha atomu kinachotokea ni ndogo kuliko jumla ya viini viwili vilivyoshiriki mle. Tofauti ya masi inabadilishwa ...

                                               

Najari (kundinyota)

Najari ni kundinyota dogo karibu na nyota angavu Kinywa cha Hutu Formalhaut. Linapakana na Dalu Aquarius na Ketusi Cetus upande wa kaskazini, Tanuri Fornax upande wa mashariki, Zoraki Phoenix upande wa kusini na Hutu Junubi Piscis Austrinus upand ...

                                               

Namba atomia

Namba atomia inataja idadi ya protoni katika kiini cha atomi. Idadi ya protoni kwakawaida huwa sawa na idadi ya elektroni za mzingo elektroni hivyo namba atomia inataja pia idadi ya elektroni. Atomi zenye namba atomia ileile ni za elementi moja z ...

                                               

Namba tasa

Namba tasa ni namba asilia isiyogawiwa kwa namba nyingine isipokuwa kwa 1 na kwa namba yenyewe. Kwa Kiingereza zaitwa "prime numbers". Mfano: 3 ni namba tasa kwa sababu inagawiwa kwa 1 na kwa 3 lakini hakuna namba nyingine inayoweza kuigawa. 4 si ...

                                               

Nambakamili

Nambakamili ni namba nzima. Inaweza kuwa chanya au hasi lakini pia sifuri, bila mchanganyiko na sehemu.

                                               

Nambamchanganyiko

Nambamchanganyiko ni namba yenye mchanganyiko wa nambakamili na sehemu. Hivyo 7 1/4 ni nambamchanganyiko.

                                               

Nebula

Nebula ni neno linalotumika kwa ajili ya kutaja eneo angavu na jeupejeupe linaloonekana angani ama kwa macho au kwa darubini. Zamani hata galaksi ziliweza kuitwa "nebula". Galaksi ya Andromeda iliyokuwa galaksi ya kwanza kutambuliwa angani ilikuw ...

                                               

Nebula ya Kaa

Nebula ya Kaa ni nebula katika kundinyota la Ngombe. Ni wingu la mabaki ya nyota nova iliyolipuka. Mlipuko wa nova ulitazamwa mwaka 1054 na kurekodiwa na wanaastronomia Wachina walioona "nyota mpya" iliyoonekana angani wakati wa mchana. Ni kiolwa ...

                                               

Ngao (kundinyota)

Ngao lipo angani kati ya makundinyota ya Kausi Mshale Sagittarius na Ukabu Aquila likigusana pia na Hayya Serpens. Lipoo karibu na ikweta ya anga.

                                               

Njia nyeupe

Njia Nyeupe, pia majarra au "mkokoto wa kondoo za Sumaili" ni jina la mlia mpana wa nyota nyingi unaoonekana angani wakati wa usiku kama wingu jeupe linalong`aa. Hali halisi hii ni jinsi tunavyoona galaksi yetu ambamo mfumo wa Jua letu pamoja na ...

                                               

Nukta

Kwa nukta kama kipimo cha wakati angalia sekunde Nukta kutoka Kiarabu نقطة, nuqta ; kwa Kiingereza: point katika elimu ya hisabati na jiografia ni kitu au mahali bila urefu wala upana, yaani bila eneo lolote. Nukta haina pande wala haiwezi kugawi ...

                                               

Nuru

Nuru ni neno la kutaja mnururisho unaoweza kutambuliwa kwa macho yetu. Kwa lugha ya fizikia ni sehemu ya mawimbi ya sumakuumeme yanayoweza kutambuliwa na jicho. Mawimbi ya nuru huwa na masafa ya nanomita 380 hadi 780 au yenye marudio ya takriban ...

                                               

Nyavu (kundinyota)

Nyavu ni kati ya makundinyota yaliyobuniwa katika enzi ya kisasa. Kama ilivyo kwa kundinyota kama ilivyo kwa nyota nyingine zinazoonekana kutoka nusutufe ya kusini pekee haikujulikana kwa Wagiriki wa Kale wala kwa Waarabu kwa hiyo wataalamu wa Ul ...

                                               

Nyotamkia

Nyotamkia ni gimba dogo la angani linalozunguka jua kwa njia ya duaradufu yenye sehemu kubwa mbali na jua na sehemu ndogo karibu na jua. Pale inapokaribia jua inaotesha "mkia" unaoipa jina lake la "nyota yenye mkia". Mkia huu ni hasa mvuke unaong ...

                                               

Ombwe

Ombwe kwa maana ya sayansi ni hali pasipo na kitu, nafasi pasipo na mata. Neno hutumiwa hasa kwa hali pasipo gesi au angahewa. Hali halisi si rahisi kupata mahali duniani pasipo kitu chochote kabisa. Mara nyingi anga-nje la ardhi yetu huitwa "omb ...

                                               

Pampu (kundinyota)

Pampu ni kati ya makundinyota yaliyobuniwa katika kipindi cha kisasa. Kundinyota hili lilielezwa mara ya kwanza na Mfaransa Nicolas-Louis de Lacaille wakati wa karne ya 18 kwa jina" Machine Pneumatique", Kilatini "Antlia Pneumatica" lililomaanish ...

                                               

Paneli ya sola

Paneli ya sola hukusanya nishati kutoka Jua kwa matumizi ya binadamu. Kuna aina mbili za paneli za sola paneli zinazokusanya joto thermal paneli za kuzalisha umeme umemenuru, photovoltaic

                                               

Paoneaanga

Paoneaanga ni taasisi ya kuangalilia anga na magimba yake kama vile jua, mwezi, nyota, sayari, kometi au galaksi. Kwa kawaida ni jengo lenye darubini kubwa. Mara nyingi hujengwa juu ya mlima au mbali na miji kwa kusudi la kupunguza athari za mach ...

                                               

Patasi (kundinyota)

Patasi lipo jirani na kundinyota za Panji Dorado na Mchoraji Pictor upande wa kusini, Saa Horologium na Nahari Eridanus, kwa maana ya mto upande wa mashariki, Arinabu Lepus, kwa maana Sungura upande wa kaskazini halafu Njiwa Columba upande wa mag ...

                                               

Pembemraba (kundinyota)

Pembemraba lipo jirani na makundinyota ya Akarabu Nge Scorpius upande wa kaskazini, Dhibu Lupus upande wa kaskazini magharibi, Bikari Circinus upande wa magharibi, Pembetatu ya Kusini Triangulum Australe upande wa kusini halafu Madhbahu Ara upand ...

                                               

Pembetatu

Pembetatu ni umbo bapa lenye pande tatu zisizonyoka na kukutana kwenye pembe tatu za kila kona. Jumla ya kiwango cha pembe zote tatu ni nyuzi 180. Eneo la pembetatu ni nusu kitako mara kimo. Pembe zatajwa kwa kawaida kwa herufi za kwanza katika a ...

                                               

Pembetatu mraba

Pembetatu mraba ni aina ya pekee ya pembetatu yenye pembe moja ya nyuzi 90°. Pembe mbili nyingine zina jumla ya nyuzi 90°. Pande zina majina maalumu kutokana na kawaida ya wanahisabati ya Ugiriki wa Kale. Pande ndefu kinyume cha pembe mraba ni hi ...

                                               

Pia

Pia ni gimba linalopatikana kama nukta zote za duara zinaunganishwa na nukta moja iliyopo juu yake. Kwa lugha nyingine pia inapatikana kama pembetatu mraba inazunguka kwenye upande wake mfupi. Eneo la duara ya msingi ni tako la nia. Umbali kutoka ...

                                               

Plastiki

Plastiki ni aina ya maunzi mango yanayoundwa kwa njia ya kikemia na kukubali umbo lolote yakiwa teke. Plastiki ni maunzi sintetiki ambayo haitokei katika mazingira kiasili. Inatengenezwa kwa kuunganisha molekuli nyingi kuwa nyororo ndefu ya polim ...

                                               

Radi

Kwa maana tofauti ya neno hili kama elementi ya kikemia angalia radi Radi pia: ngurumo ya umeme ni mwangaza na miale ya mwanga mithili ya shoti za umeme inayotokea wakati wa ngurumo wa mvua ya radi. Neno radi linaweza kutaja pia sauti yenyewe na ...

                                               

Risasi

Kwa elementi na metali angalia Risasi Risasi ni gimba dogo la metali linalorushwa kutoka kasiba ya bunduki. Mara nyingi risasi hutengenezwa kwa plumbi yaani metali inayoitwa pia "risasi". Jina la metali imekuwa jina kwa ajili ya silaha.